Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
ametuma risala za rambi rambi kwa familia za wale waliouawa katika
shambulizi la chuo kikuu cha Garissa kazkazini mashariki mwa
Kenya.Kiongozi huyo vilevile amewahakikishia wakenya kwamba serikali
yake imechukua hatua za kuwapeleka maafisa wa usalama katika eneo
hilo.Amewataka wakenya kuwa watulivu wakatu huu ambapo maafisa wa
usalama wanakabiliana na wapiganaji hao.
17.00pm:Waziri wa usalama Kenya:
Waziri
wa maswala ya ndani nchini Kenya Joseph Nkaiserry amethibitisha kuwa
watu 15 wameuawa huku wengine 53 wakijeruhiwa kufuatia shambulizi la
alfajiri katika chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya.miongoni mwa
waliokfariki ni walinzi wawili wa mlango wa chuo hicho.Akizungumza
kutoka Garissa Nkaiserry amesema kuwa oparesheni ya kuwasaka wahalifu
hao itaendelea hadi mateka wote waokolewe.
16.50pm:Mshukiwa mkuu:
Serikali
ya Kenya imemtaja Mohammed Kuno kama mshukiwa mkuu aliyepanga njama za
shambulizi la chuo kikuu mjini Garissa.Katika taarifa kwa vyombo vya
habari waziri wa usalama nchini Kenya Joseph Nkaiserry alitoa zawadi ya
dola 53,000 kwa mtu yeyote atakayemkamata mshukiwa huyo ama kutoa habari
zake.Kuno anajulikana kama 'Gama'adhere kwa jina maarufu.
Post a Comment