Yanga waikomoa Simba. Sh 1.7 bilioni yatakiwa kulipwa.. Soma habari kamili hapa
YANGA itaifungulia Simba kesi ya madai ya dola milioni moja sawa na Sh 1.7 bilioni kiasi ambacho timu ya Wadi Degla FC ya Misri nayo itatakiwa kulipa kama Yanga ikishinda kesi kwa hoja inazojenga.
Yanga inataka straika, Emmanuel Okwi raia wa Uganda asijihusishe na masuala ya soka kwa kipindi kisichopungua miaka mitano.
Pia, rungu hilo limemwangukia straika wao wa
zamani, Mbrazili Genilson Santos ‘Jaja’ ambaye wanataka awalipe dola
56,000 sawa na Sh97 milioni ambapo kati ya pesa hizo, dola elfu 20 sawa
na Sh 35 milioni ni fidia ya pesa za usajili alizochukua na dola 36,000
sawa na Sh63 milioni ni pesa za mshahara wa miezi 12, wakati Juma Kaseja
anatakiwa alipe kiasi cha Sh300 milioni fidia ya pesa za usajili na
Sh26 Mil kama sehemu ya mshahara wake wa miezi 12 ambayo imebakia kwenye
mkataba wake na Yanga.
Mkuu wa Idara ya Sheria katika klabu ya Yanga,
Frank Chacha, alitolea ufafanuzi wa suala hilo kwa Mwanaspoti jana
Jumatatu, katika ofisi za Makao Makuu ya Klabu hiyo Jangwani jijini Dar
es Salaam kuwa, yamefikia mahali pazuri na hadi kufikia mwezi Machi
mambo yatakuwa yameshakamilika.
Alisema: “Suala la Okwi, tutafungua kesi ya madai
Fifa tunataka afungiwe kujihusisha na shughuli za michezo kwa kipindi
kisichopungua miaka mitano. Pili atulipe kiasi cha dola Milioni 1 (sawa
na Sh1.7 bilioni) kama fidia ya kuvunja mkataba na dola 100,000 kwa
ajili ya gharama za huduma tulizompa kama kufundishwa mazoezi na mambo
mengine.
“Pia klabu zilizohusika kama Simba na Wadi Degla
kila moja inatakiwa kulipa dola milioni moja (sawa na Sh. 1.7 bilioni)
Wadi Gegla inahusika kwa sababu wameingilia mkataba walipozungumza na
Okwi ukiwa bado mrefu, wakati Simba ndiyo klabu anayoichezea sasa,
amejiunga wakati mkataba wake ukiwa mwanzoni,”alisema Chacha..
“Na Jaja ambaye alibaki kwao kwa madai ana
matatizo ya kifamilia na baadaye akakaa kimya tu hadi leo hii bila
taarifa yoyote na sasa kuna timu anaichezea, tutamfungulia kesi Fifa ya
kumdai fidia ya dola elfu 20 (sawa na Sh35 Mil) pamoja na dola elfu 3
mara 12 (sawa Sh63 Mil) ikiwa ni sehemu ya mshahara wake kwa muda wa
mwaka mmoja,”alisema Chacha.
Chacha alikwenda mbali na kulitolea ufafanuzi
suala la Kaseja na kusema, watamfungulia kesi mahakama ya kazi: “Kaseja
anatakiwa kuilipa Yanga Sh300 Mil, hiyo ni fidia ya kuvunja mkataba na
Sh2.2 Mil mara 12 ikiwa ni sehemu ya mshahara wake kwa muda wa mwaka
mmoja uliokuwa umebaki katika mkataba wake.”
Amesema, Kaseja alituma barua ya kutaka kuvunja
mkataba kwa sababu ya mambo matatu ambayo ni kutomaliziwa pesa ya
usajili Sh20 Mil, hakupata nafasi ya kucheza na tatu hakukatiwa bima ya
majeruhi, lakini wao walimfafanulia kila kitu.
Lakini alituma barua ya kuvunja makataba Novemba
11 mwaka 2014 wakati pesa zake za usajili zilikuwa zimeshatumwa tangu
Oktoba 27, 2014 kwa maana hiyo yeye ndiye alivunja mkataba.
Chacha aliendelea na kusema, watawafungulia kesi
ya madai ya zaidi ya Sh100 milioni wanachama; Wema Chikota, Juma Mtibwa
na Kingwamba Kingwamba ambao walifungua kesi ya kupinga katiba ya Yanga
ya mwaka 2010 na kuitambua ile ya mwaka 1968.
Post a Comment