Mbio zamwokoa mwamuzi uwanjani
MBIO za mwamuzi, Ezekiel Ngoji, wa Shinyanga juzi Jumapili
zilimwokoa asipate kipigo cha nguvu kutoka kwa wachezaji wa Polisi
Dodoma baada ya kutokea vurugu kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza
dhidi ya Toto African katika Uwanja wa Kirumba jijini hapa.
Vurugu hizo ambazo zilifanya Polisi waliokuwepo uwanjani hapo kufyatua mabomu ya machozi kadhaa kuthibiti hali hiyo.
Awali mchezo ulianza vizuri lakini hali
ilibadilika kipindi cha pili kwenye dakika ya 63 baada ya mwamuzi Ngoyi
kutoa penalti kwa Toto kwa kile kilichoelezwa kipa wa Polisi Madopi
Mwingira alimchezea rafu mmoja wa washambuliaji wa Toto.
Penalti hiyo ilipigwa na Hamim Abdul ambaye
alifunga na sekeseke lilianza baada ya mwamuzi huyo kumtoa kwenye benchi
mmoja wa makocha wa Polisi na ndipo vurugu hizo zilipoanza kwa mmoja wa
wachezaji wa Polisi kuanza kumshambulia mwamuzi Ngoyi.
Baada ya kuona hivyo mwamuzi huyo alitimua mbio
kuelekea jukwaa kuu kujiokoa na kipigo hicho hali iliyowafanya askari
waliokuwepo uwanjani hapo kufyatua mabomu ya machozi kuzuia vurugu hizo.
Dakika 20 baadaye, waamuzi hao walitoka jukwaa kuu
wakiwa na maofisa wa Polisi na viongozi wa Chama cha Soka Mkoa wa
Mwanza(MZFA)na kwenda uwanjani kupiga kipenga cha kumaliza pambano.
Kocha wa Polisi Dodoma, Gabriel Marwa alisema
mwamuzi wa mezani ndiye aliyeharibu pambano kwa kuwatoa bila sababu
kwenye benchi viongozi wenzake jambo lililosababisha hali hiyo.
Post a Comment