Sasa ni ujio wa Thiery Henry ndani ya Bongo. Hii ndio ratiba yake..


Mkurugenzi wa maendeleo na mahusiano wa klabu ya Arsenal ya England Sam Stone (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa uwekezaji wa klabu hiyo nchini,kushoto ni meneja wa kitengo hicho Daniel Willey


MABOSI wa klabu ya Arsenal jana Jumatatu walianza vikao na makampuni 20 ya Tanzania katika kutaka kujenga uhusiano, lakini katika safari yao hiyo wametamka kwamba wanakusudia kupandisha soka la hapa nchini kwa kuwaleta makocha wao na wachezaji wao nguli waliopita.
Akizungumza jijini jana Mkurugenzi wa Maendeleo na Uhusiano wa Nje wa klabu hiyo, Sam Stone, alisema Arsenal imekusudia kufanya kazi na makampuni mbalimbali katika upande wa Biashara na soka ambapo katika mpango huo makocha mbalimbali wa timu za vijana wa klabu zao watatua nchini kusaka vipaji.
Stone aliyeambatana na meneja wa kitengo hicho Daniel Willey alisema mbali na ujio wa makocha hao ambao utaambatana na kuanzisha promosheni maalum kwa mashabiki kuzuru uwanja wao wa Emirates pia wachezaji wao wa zamani akiwemo nguli Thierry Henry na Robert Pires pia watapata fursa ya kuja nchini kuangalia maendeleo ya soka.
“Arsenal ipo tayari kuleta makocha hapa kama kila kitu kitakuwa sawa kuangalia nini kinaweza kufanyika katika kuboresha soka la vijana wadogo, lakini pia hata wale wachezaji wetu wa zamani wanaweza kuja hapa kama alivyokuja Pires pale Uganda.

No comments