Msuva afichua ukweli wake Yanga




MSHAMBULIAJI wa Yanga, Simon Msuva, ametoa dukuduku lake la moyoni kuwa anapenda kwenda kucheza soka nje ya nchi, lakini tatizo lake hajapata wakala wa kumtafutia nafasi hiyo.
Msuva ambaye anafanya vizuri kwenye mpira wa Tanzania kwa sasa, wadau wengi wa soka wanaamini alipofikia sasa, ana nafasi ya kutoka na kucheza mpira wa mafanikio nje ya nchi, lakini bado wanamwona Yanga.
Ndipo akafunguka na kuliambia Mwanaspoti akisema: “Nafanya vizuri na malengo yangu ni kutoka kucheza mpira wa ushindani nje ya nchi, lakini nataka watu watambue kuwa sijapata wakala wa kunitafutia timu.
“Sina mtu ambaye anaweza kuniongoza na kunitafutia timu tofauti za majaribio kama ilivyo kwa wenzangu kama nikipata. nitashukuru sana.
“Nikipata timu kutoka nchi yoyote niko tayari, sichagui kwa kwenda lakini kwa kuanzia napenda sana kucheza Afrika Kusini.”
Alisema anatamani namna anavyosikia wachezaji wenzake kama, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta wanaokipiga klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo naye aje kufanikiwa siku moja.

No comments