STRAIKA wa Yanga, Danny Mrwanda, anakatiza kilometa kadhaa katika mitaa ya Bagamoyo ambako wameweka kambi akifanya mazoezi binafsi kuhakikisha anaendeleza kasi yake ya kufunga mabao na kumshawishi kocha wake, Hans Van Der Pluijm, awe anampanga kikosi cha kwanza kila mechi.
Mrwanda tayari ana mabao manne katika Ligi Kuu
Bara msimu huu na yote aliyafunga alipokuwa Polisi Moro, tangu
alipojiunga na Yanga katika usajili mdogo hajafunga bao hata moja huku
akiingia na kutoka kikosi cha kwanza.
Yanga ipo kambini Bagamoyo ikijiandaa na mechi ya kesho ya dhidi ya Ruvu Shooting.
Mrwanda anayewania nafasi na Amissi Tambwe, Kpah
Sherman, Hussein Javu na Jerry Tegete, alisema: “Ushindani wa namba
umekuwa mkubwa, kwa mchezaji anayejitambua ni lazima apambane.
Ninakimbia barabarani kila asubuhi ili niwe imara.”
Mabao yake manne yanamweka katika nafasi ya pili
kwa ufungaji nyuma ya Mrundi wa Azam FC, Didier Kavumbagu aliyefunga
mara tano. Wengine wenye mabao manne ni Rama Salim (Coastal Union), Ame
Ally (Mtibwa), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Simon Msuva (Yanga).
Post a Comment