Kabadeni atoa onyo kwa Boban, Cannavaro na Bathez
KOCHA wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni,
amewatolea uvivu wachezaji wanaojipachika majina ya nyota wa Ulaya kwa
kuwaambia waache tabia hiyo kwani ni aibu kwao kwani wengi wanafanya
madudu uwanjani.
Kibadeni alisema anashangazwa na
ulimbukeni unaofanywa na wachezaji hao kulewa sifa kwa kuitwa majina ya
mastaa wa nje wakati viwango vyao haviendani na na vya mastaa hao jambo
libalodhihirisha kuwa hawana mwelekeo wa kufika mbali.
“Inashangaza mchezaji kujiita
Mario Balotelli (straika wa Liverpool), siku akienda Ulaya ataitwa
nani? Ni aibu kwa wachezaji wa Tanzania wabadilike,” alisema Kibadeni.
Alisema wakati yeye anaichezea
Simba kulikuwepo na mshambuliaji Sunday Manara aliyepewa jina la
‘Computer’ kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao wakati huo, huku yeye
akijiita ‘King’ yote yaliendana na kazi zao na si vinginevyo.
Wachezaji wanaotumia majina ya
mastaa wa nje kuliko ya kwao ni Ally Mustapha ‘Barthez’ (Yanga)
akifananishwa na kipa wa zamani wa Ufaransa, Fabian Barthez, beki Nadir
Haroub ‘Cannavaro’ anayefananishwa na beki wa zamani wa Italia, Fabio
Cannavaro na Haruna Moshi ‘Boban’ wa Friends Rangers anayefananishwa na
Zvonimir Boban wa Croatia.
“Sisi tulikuwa tukifanya mazoezi hata saa saba za usiku ili tutishe uwanjani, si hawa,” alisema Kibadeni.
Post a Comment