Jinsi Arsenal ilivyoisambaratisha Man City


Timu ya Arsenal imeichabanga timu ya man ciity Bao 2 bila majibu katika mchezo wa ligi kuu Uingereza uliopigwa kwenye Dimba la Etihad.Arsenal ambao walikua na kasumba mbaya kila wakutanapo na timu
kubwa walivunja mzizi wa fitina angali wakicheza kwenye kiwanja cha ugenini.Shukrani zimuendee Santiago Cazorla aliyefunga bao la kwanza dakika ya 24  kwa mkwaju wa penati baada ya Kompony kumuangusha beki Monreal.Cazorla alitengeneza tena bao la pili la Arsenal lililofungwa na Olivier Giroud.Ushindi huo umerejesha imani na matumaini kwa washabiki wa Arsenal kurudi kwenye timu 4 za juu

No comments