Huyu ndiye Beki king’ang’anizi atakayetua Simba
UNAPOZUNGUMZIA mabeki wa kati wenye uwezo mkubwa kwenye Ligi Kuu Bara, lazima awepo Salim Mbonde wa Mtibwa Sugar.
Mbonde ni chipukizi mwenye umri wa miaka 21 na
juhudi zake uwanjani ndizo zimefanya jina lake litambulike kwa haraka
kwenye soka nchini, sasa ni kati ya mabeki ghali Tanzania.
Mbonde amejaliwa umbo kubwa lililojengeka
kimichezo na ni mrefu achezapo soka hutumia akili na nguvu kama ilivyo
kwa mabeki wengine.
Sh15 Milioni zitamng’oa Mtibwa
Nyota huyo alianzia mbali kusaka mafanikio na sasa
hali ya kijana ni tofauti. Hata hivyo licha ya kusogelea malengo yake
bado anaendelea kutafuta.
Anafahamu maisha magumu aliyopitia na sasa
anajitambua na anajiamini na huenda elimu aliyoipata inamsaidia kupanga
na kufanya maamuzi sahihi.
Kabla ya kuanza kwa msimu huu, klabu kadhaa
zilimuhitaji lakini kutokana na kujitambua kwake kwenye makubalino ya
maandishi, ametamka kuwa timu itakayotaka kumng’oa kwenye kikosi cha
Mtibwa lazima ijiandae katika dau la usajili.
Atasaini makataba kwenda timu nyingine kwa dau
lisilopungua Shilingi 15 milioni ingawa kwa sasa katika timu yake ya
Mtibwa anacheza kwa fedha ambayo ni chini ya hapo.
“Maisha ni malengo, kama unavyojua maisha ya soka
ni mafupi ukicheza hapa mwanzoni baadaye itakuwa shida,” anasema Mbonde
ambaye alianza soka katika timu yake ya mtaani ya Uhuru Rangers ya
Morogoro na baadaye akajiunga na akademi ya Moro Youth chini ya makocha
Hussein Mau na Alan Figo, hapo alicheza kwa miaka mitatu na kwenda JKT
Oljoro na baadaye Mtibwa.
“Malengo yangu ni kucheza mpira wa mafanikio ndiyo
maana napambana na habari za usajili wapo wanaohama na baadaye wanakuja
kujutia.
“Naweza kucheza timu yoyote lakini nimejipangia
dau la usajili, nitasajili timu nyingine kulingana na makubalino.
Nitaondoka Mtibwa kama nikipewa Sh15 milioni ingawa kwa Mtibwa naweza
kusaini chini ya hapo.
“Nasema hivyo kwa sababu naiheshimu Mtibwa, imenitoa mbali, nina amani ninaishi vizuri, napata kila kitu.
Post a Comment