Haya maneno ni ya kweli?
MSHAMBULIAJI wa Simba Dan Sserunkuma amefungua akaunti yake ya mabao katika Ligi Kuu Bara juzi dhidi ya Ndanda ya Mtwara, lakini kocha wa Wekundu hao Goran Kopunovic ameibuka na kusema sasa timu ambazo hazijakutana na Simba kazi wanayo.
Akizungumza na Mwanaspoti, Kopunovic alisema
mabadiliko ya uchezaji ambayo sasa Sserunkuma anayo yaliyomwezesha
kufunga bao la kwanza katika ushindi wa 2-0 juzi Jumamosi, yatampa
makali zaidi katika mechi zijazo za timu hiyo.
Kopunovic alisema alikuwa na imani kubwa na
Sserunkuma licha ya kushindwa kufunga katika mechi saba za awali
alizoichezea Simba na sasa kitendo cha kufunga bao hilo kinamwongezea
imani hiyo huku kikimpa ujasiri mchezaji huyo hali inayomrudishia uwezo
wa kujiamini zaidi uwanjani.
Alisema mbali na uwezo wa Sserunkuma, pia
amefurahishwa na hali ya kupambana kwa wachezaji wake ambapo sasa
wanarudi jijini Dar es Salaam kuanza maandalizi rasmi ya kuwaandalia
kichapo Azam FC ambao watakutana nao Jumamosi.
“Dan (Sserunkuma) ni mchezaji mzoefu ambaye licha
ya kwamba awali alikuwa hafungi, lakini sikuwa na wasiwasi nay,” alisema
kocha huyo.
“Nilikuwa naamini kuwa ataanza kufunga muda si
mrefu na kweli imekuwa hivyo, sasa amefunga na ninaamini atakuwa mwiba
mkali kwa timu zote ambazo tutakutana nazo sasa katika ligi.”
Post a Comment