MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Ally Shiboli, ambaye kwa sasa
anakipiga African Sport ya Tanga inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza,
ameweka wazi sababu iliyomshusha kiwango alipokuwa na Wekundu wa
Msimbazi akisema ni kuchanganywa na mwanamke aliyekuwa mchumba wake.
Akifafanua tukio hilo Shiboli, alisema alijikuta
anatoka katika hali ya mchezo baada ya mchumba wake huyo aliyekuwa
anamhudumia kila kitu kama mke, kumsaliti na kuchukuliwa na rafiki yake.
“Nakumbuka niliitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars
tulienda kucheza Msumbiji niliporudi nikakuta yule mwanamke kabadilika
tabia na mimi nilikuwa nimewekeza kwake, ilinifanya niumie hadi
nishindwe kufanya vema katika timu yangu,” alisema.
Lakini anazungumzia maisha yake kisoka ya sasa
kuwa ameamua kuweka kando suala zima la wanawake badala yake yupo katika
harakati za kusaka nafasi ya kurejea katika timu zinazocheza Ligi Kuu
Bara.
“Baada ya maumivu yangu kuisha niliamua jambo
moja, kwanza kuna magonjwa, pia lazima nijenge maisha yangu mwenyewe na
kama ni mke nitampata tu yule anayejitambua kwa hiyo kwa sasa
nimeelekeza nguvu zangu katika soka sitaki kabisa kusikia ujinga wa
mademu,” alisema.
Post a Comment