Coutinho alianzisha kasheshe jingine Yanga..




ANAPENDA masihara wakati mwingine. Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Mbrazil Andrey Coutinho, ametoa kali ya mwaka, ambapo amewataka mabeki wa Yanga wakiongozwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuhakikisha wanacheza mchezo wa vurugu wanapokuwa mazoezini ili viungo na washambuliaji wa timu hiyo wapate uzoefu wa kukabiliana na mabeki wasumbufu, wakorofi wa timu nyingine.
Coutinho aliliambia Mwanaspoti akisema: “Kuna haja ya kuwa na mazoezi ya aina hiyo hasa kwa mabeki wetu.
“Tukiwa mazoezini wanatakiwa kucheza kibabe, lakini pia wanatakiwa kucheza na saikolojia ya mchezaji kama walivyo mabeki wa timu zingine. Kama
tukiweza kutekeleza hilo basi tutaweza kupambana na timu yoyote yenye mabeki wanaokamia na kucheza rafu mbaya.
“Ninajua kiuhalisia si vizuri kwenye soka kucheza kibabe kwani kuna sheria za soka. Lakini ni vyema kujiandaa na hali halisi ilivyo.”
Kiungo huyo pia ametamka wazi kuwa anataka kuhakikisha msimu huu Yanga inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na hatimaye kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.

No comments