SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeitaka Simba kuwa makini na uamuzi wao wa kusitisha mikataba ya wachezaji wake na kukumbushwa kesi yao dhidi ya beki Mkenya Donald Mosoti ambaye aliishitaki Simba Fifa kwa kuvunja mkataba wake pasipo makubaliano yoyote.
Wiki hii Simba ilimsainisha mkataba wa miaka miwili straika Dan Sserunkuma aliyekuwa Gor Mahia ya Kenya na kutangaza kusitisha mkataba na mshambuliaji wao Mkenya Raphael Kiongera ambaye yupo India ambako amekwenda kufanyiwa upasuaji wa goti.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, alidai wamesitisha mkataba wa Kiongera ambaye atakaa nje kwa zaidi ya miezi miwili baada ya kufanyiwa upasuaji na wataendelea naye msimu ujao, ingawa Kiongera aliliambia Mwanaspoti kuwa hawajazungumza lolote kuhusu mkataba wake.
Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, alisema: “Usajili wa Sserunkuma tunausikia tu, tunasubiri watakapowasilisha usajili wao, Simba na klabu nyingine zinatakiwa kufuata taratibu zote za usajili na uvunjaji mikataba ili kuepuka kesi, kumbuka Simba wana kesi na Mosoti
Post a Comment