TAMBWE AANZA HIVI
STRAIKA namba moja wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Amissi
Tambwe, ameanza tizi kwa morali ya nguvu kwenye klabu hiyo na kumshtukia
kocha anayesubiri barua yake ya kufutwa kazi, Marcio Maximo sambamba na
Msaidizi wake, Leonardo Neiva.
Tambwe ambaye si chaguo la Maximo, alipiga tizi
kwa mara nyingine jana Alhamisi kwenye Uwanja wa Loyola, Dar es Salaam
huku akipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wachezaji wenzake ambao
wanaamini kwamba anaweza kuiziba mdomo Simba kwa kutumbukiza idadi kubwa
ya mabao kuliko yale 19 aliyotupia akiwa Msimbazi msimu uliopita.
Wachezaji hao, makocha pamoja na wachambuzi wa
soka wanadai kwamba Simba itajuta kuiuzia Yanga silaha. Katika mazoezi
hayo, Maximo ambaye alisimama pembeni alikuwa akimfuatilia kwa karibu
zaidi Tambwe na kumtathmini na kumshika mkono baadaye ingawa hakutaka
kumzungumzia kwa lolote, aligoma pia kuzungumzia sakata lake.
Akizungumza na Mwanaspoti Tambwe ametamba
kufumania nyavu na kutetea ufungaji bora wa Ligi kwa msimu pamoja na
kuipa Yanga ubingwa ikiwa ni njia moja ya kuthibitisha ubora wake.
“Nina nafasi ya kufunga zaidi kuliko msimu
uliopita kutokana na mfumo wanaotumia Yanga, lakini pia aina ya
wachezaji waliopo Yanga. Ninajiamini na ninafuraha ya kujiunga na Yanga,
Naamini nitaweza kufanya kazi kubwa kwa kuwa nimetambulika Yanga kwa
kazi nzuri niliyokuwa nikiifanya Simba siku za nyuma,” alisema Mrundi
huyo.
“Kipindi cha mwisho nikiwa Simba sikuwa na furaha,
iwe kwenye ligi au hata kwenye mazoezi, lakini sasa najiona nina amani
na nitaweza kufanya kazi kubwa, kwa kushirikiana na wenzangu ninataka
kuhakikisha ninashinda Kiatu cha Dhahabu lakini pia kuhakikisha Yanga
inachukua ubingwa.
“Naamini kwa mfumo na kasi walizonazo wachezaji wa
Yanga, nitaweza kufunika kwenye ufungaji mabao. Mpaka sasa anayeongoza
ana mabao manne, mimi nina bao moja hivyo sipati shida kupambana na
kupata mabao mengi na kuwapiku waliopo juu yangu.”
straika huyo amewaomba mashabiki wa Simba wasimchukie kwa kucheza kwake Yanga kwa vile viongozi wa Simba ndio waliomfukuza.
Tambwe amejiunga na Yanga akitokea Msimbazi baada ya kuachwa na klabu hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa ameshuka kiwango.
Mrwanda amsifu Tambwe
Danny Mrwanda amemwangalia Tambwe katika mazoezi
yao namna anavyojituma na kutamka: “Nimemwangalia Tambwe katika mazoezi
yetu kwa siku hizi chache, jamaa yupo vizuri na ameifanya safu ya
ushambuliaji iwe na ushindani zaidi. Ana uwezo katika kufunga, anajituma
na anajua anachokifanya,
Post a Comment