HIKI NDICHO KILICHOMTOA MAXIMO YANGA




LAITI kama angejua asingekubali kurudi tena nchini na kufanya kazi na Yanga.
Angeacha Watanzania waendelee kumheshimu kama kocha wa aina yake aliyepata kutokea nchini.
Angebaki na sifa yake ya kuwa mhamasishaji mzuri aliyewafanya Watanzania kuipenda timu yao ya taifa.
Angebaki kuwa na sifa ya kuifikisha Tanzani kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya wachezaji wa ndani (chan) mwaka 2009 nchini Ivory Coast.
Kama asingekuja angekuwa amefanikiwa kuuficha udhaifu wake ambao umeonekana pindi aliporudi kwa mara ya pili kuifundisha Yanga.
Kwanza, imebainika kwamba Maximo bado ni muoga wa kufungwa, anayetegemea sana kucheza kwa mtindo wa kulinda zaidi lango lake.
Hawezi kufanya usajili wa kuiwezesha timu kufanya vizuri na hana jicho la kuchagua wachezaji wa kuweza kuisaidia timu.
Mfano ni pale alipotoa ripoti yake kwa viongozi wa Yanga na kuwapendekeza wachezaji Jabir Azizi na Shaaban Nditi kuwa wanafaa kusajiliwa na Yanga.
Pia, kocha huyo alitangaza kwamba usajili wa mchezaji mmoja utakuwa ‘surprise’ kwa wapenzi wa soka na ilipokuja kubainika kuwa mchezaji wenyewe ni Danny Mrwanda! Kila mtu alishangaa.
Sina nia ya kumponda Mrwanda, lakini kwa wapenzi walioanza kushabikia soka katika miaka ya 70, Mrwanda si ‘surprise’ kwa Yanga.
Mrwanda ni mchezaji aliyesajiliwa Yanga kutokana na siasa za Simba na Yanga, wala sidhani kama hilo ni ajabu, utasemaje usajili wa Amissi Tambwe kama huo wa Mrwanda ni ‘surprise’?
Maximo ana akili za kukariri, amekariri majina ya wachezaji waliokuwa wakifanya vizuri katika kipindi chake alipokuwa akifundisha timu ya taifa!
Pia, ujio wake wa mara ya pili, ameonyesha kuwa Maximo ni mbinafsi, ambaye anawapendelea sana Wabrazili wenzake.
Kwa Geilson Santos ‘Jaja’maji yalizidi unga, hakuwa na budi kumwambia aachie ngazi mapema asije kumwagia kitumbua chake mchanga.
Siyo kweli kwamba, Jaja alikuwa na matatizo ya kifamilia, bali Maximo alishtuka baada ya kuwaona Watanzania wamemshtukia kuwa hakuwa mchezaji wa kiwango kinachostahili kuichezea Yanga.
Pamoja na kwamba, Andrey Couthino ni mchezaji wa kawaida sana, lakini kocha huyo aliona angeweza kuendelea naye kuliko kubaki na Jaja ambaye alikuwa akipingwa sana.
Lilipokuja suala la kumpunguza mchezaji mmoja wa kigeni kati ya Hamis Kiiza na Coutinho, hapo ndipo Maximo alipoonyesha ubaguzi wake.
Ni mwendawazimu tu anayeweza kumwacha Kiiza na kuendelea na Coutinho!
Sijui kwa nini Maximo alikuwa akimchukia Kiiza, inawezekana jina la utani la mchezaji huyo la Diego lilichangia, kwani Wabrizili na Waajentina huwa hawaivi kwenye soka.
Unamkumbuka kocha wa Simba Mbrazili Silva? Mwaka 1982 kocha huyo alikuwa akimweka benchi Malota Soma kwa sababu tu alikuwa akifananishwa na Maradona.
Hali hiyo ilimfanya kumwingiza katika dakika 10 za mwisho, kama Maximo alivyokuwa akifanya kwa Kiiza.
Hii ni hulka ya Mbrazili, jambo dogo kama hilo kwao ni kubwa sana kutokana na upinzani wao na taifa la Argentina.
Pamoja na viongozi wa Yanga kukubali kumuondoa Kiiza kutokana na ushauri wake, bado Maximo alikataa ushauri wa viongozi hao walipomtaka kumuondoa, msaidizi wake, Leonard Leiva na nafasi hiyo kupewa mzawa Charlse Boniface Mkwasa.
Kuna siri gani hapa? Maximo alikuwa akimtumia Leiva kama mtu wake wa kumfichia udhaifu wake kuifundi.

No comments