Salamu za Ivo Mapunda kwa Yanga

Kuifunga Yanga kumetupa matumaini- Ivo Mapunda.
Mapunda alisema dhamira yao kubwa ni kubadili mwenendo kwa kupata ushindi katika mechi za Ligi Kuu


KIPA wa Simba Ivo Mapunda amesema ushindi wa mabao 2-0 walioupata dhidi ya wapinzani wao Yanga utawasaidia waweze kupata matokeo mazuri kwenye Ligi Kuu Tanzania bara ambayo kwa sasa ipo katika raundi ya nane.
Mapunda alisema dhamira yao kubwa ni kubadili mwenendo kwa kupata ushindi katika mechi za Ligi Kuu ili kufufua matumaini ya ubingwa kama ambavyo wamejipangia msimu huu.
“Nafahamu kuwafunga Yanga siyo kuwa mabingwa wa Tanzania bara msimu huu lakini kwa kiasi fulani umetufanya tujione tunaweza hata kuwa mabingwa kwa sababu mashabiki na viongozi wetu pia wamepata matumaini makubwa,”amesema Mapunda.
Mapunda ameidakia Simba mechi mbili tu msimu huu kati ya saba za ligi ilizo cheza timu hiyo inayoshikilia nafasi ya saba kwenye msimamo ikiwa na pointi tisa sawa na timu za Stand United, Polisi Moro na Mgambo JKT

No comments