Kwa mikakati hii, Lazma tuipe Yanga Ubingwa- Boniface Mkwasa
Mkwasa ameungana na Pluijm kwa mara ya pili kuchukua nafasi za Wabrazili Marcio Maximo na msaidizi wake Leonaldo Neiva
KOCHA saidizi wa Yanga Boniface Mkwasa, ameiambia Goal, kuwa lazima waipe timu hiyo ubingwa wa Vodacom Tanzania bara baada ya uzoefu mkubwa walioupata msimu uliopita walipomaliza nafasi ya pili nyuma ya Azam.
Mkwasa aliyeungana na Pluijm kwa mara ya pili kuchukua nafasi za Wabrazili Marcio Maximo na msaidizi wake Leonaldo Neiva walisitisha mikataba yao na Yanga na kujiunga na timu ya Al Shaula, inayoshiriki Ligi Kuu nchini Saudi Arabia.
“Tunatambua ushindani uliopo kwenye ligi yetu hivi sasa lakini tumejipanga kuhakikisha tunakabiliana nayo na msimu huu Yanga inakuwa bingwa baada ya kumaliza nafasi ya pili msimu uliopita,”alisema Mkwasa.
Mkwasa alisema tangu waaze kazi wamekuwa wakifanya kazi ya kurudisha juu ari ya wachezaji ili waweze kufanya vizuri katika mechi zinazo kuja ikiwemo ile ya Jumapili dhidi ya Mabingwa watetezi Azam FC
Post a Comment