Endapo Yanga watafanikiwa kuwatoa BDF IX inatarajia
kupambana na Sofapaka ya Kenya au Platnum ya Zimbabwe
WASHINDI wa pili wa Ligi ya Vodacom Tanzania bara msimu uliopita Yanga imepangwa kucheza na timu ya BDF IX ya Botswana katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika CAF.
Kwa mujibu wa Mtandao wa CAF, mechi hiyo zitafanyika mwezi Februari na Yanga itaanzia nyumbani uwanja wa taifa Dar es Salaam kati ya tarehe 13 na 15 na mchezo wa marudiano utafanyika Gabrone Botswana kati ya tarehe 27 na Machi 2.
Kocha Hans Pluijm anayekinoa kikosi cha Yanga kwa sasa ameiambia Goal kuwa ratiba hiyo ni nzuri kwakua imewapa muda mrefu wa kujiandaa hadi kufikia huko.
Yanga imeingia kambini leo kwenye Hoteli ya Kiromo Bagamoyo kujiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya mabingwa watetezi Jumapili ijayo.
Endapo Yanga watafanikiwa kuwatoa BDF IX inatarajia kupambana na Sofapaka ya Kenya au Platnum ya Zimbabwe.
Post a Comment