Kilichosababisha Simba yetu ianze ligi kwa mfululizo wa suluhu

“Uchanga wa kikosi sababu Simba kuanza Ligi Vibaya” – Evans Aveva.


Kuanza vibaya kwa timu hiyo msimu huu kumetokana na uchanga wa kikosi walichoanza nacho ligi ya msimu huu ambacho kinatumia zaidi ya asilimia 50 ya wachezaji vijana
RAIS wa klabu ya Simba Evans Aveva Amsema kuanza vibaya kwa timu hiyo msimu huu kumetokana na uchanga wa kikosi walichoanza nacho ligi ya msimu huu ambacho kinatumia zaidi ya asilimia 50 ya wachezaji kutoka kikosi cha timu yao ya vijana wenye umri chini ya miaka 20.
Akiongea na Goal Aveva alikiri kuwa nafasi ya saba ambayo inashikwa na timu yake kwenye msimamo wa Ligi Kuu haiendani na hadhi ya klabu hiyo kongwe lakini alisema hiyo ilitokana na matatizo mbalimbali ambayo uongozi wake uliyakuta kutoka awamu iliyopita iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Ismail Aden Rage.
“Kuanza kwetu vibaya msimu huu kumetokana na vitu vitatu ambavyo haikuwa rahisi kuviepuka chakwanza ni uchanga wa kikosi chao ambacho kinatumia wachezaji zaidi ya aslimia 50 kutoka timu yao ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 hivyo walihitaji kuvumiliwa kwakua ilikuwa ni kipindi cha mpito,”amesema Aveva.
Aveva pia ametangaza Kamati 10 na kuzungumzia matumaini ya kujenga uwanja wa Bunju ambao hadi sasa wameshapokea michoro kutoka kwa kampuni ya Envirok na kutakiwa kutafuta bilioni 2.5 ili kufanikisha ujenzi wa uwanja na Hosteli .

No comments