Nani atakuwa mrithi wa jezi ya Yaya Toure Man City?

Yaya Toure 

MEI 31 mwaka huu, kiungo wa Manchester City, Yaya Toure ametimiza umri wa miaka 31. Ni wazi kwamba umri wake umeanza kumtupa mkono na muda wowote kuanzia sasa Yaya ataanza kwenda chini.
Kwa sasa anasumbuliwa na majeruhi na kuna mechi ambazo zimeanza kumuelemea. Nani atarithi kiti chake endapo ataondoka?
Paul Pogba (Pauni 45 milioni)
Siku zote Manchester City imeendelea kuhusishwa na uhamisho wa kiungo huyu wa kimataifa wa Ufaransa. Ana urefu kama Toure na ana mwili kama Toure.
Akiwa na umri wa miaka 21 tu, Pogba ni mmoja kati ya viungo waliokuja juu barani Ulaya huku akiwa na namba ya kudumu katika kikosi chake cha timu ya taifa na klabuni Juventus. Aliondoka Manchester bure baada ya timu hiyo kushindwa kuafikiana naye kuhusu mkataba mpya lakini kwa sasa thamani yake imepanda kufikia Pauni 40 milioni.
Wakati Yaya akiwa anatumia nguvu zaidi, Pogba ni mchezaji anayetumia nguvu na akili na amekuwa akifunga zaidi mabao ya mashuti. Kama akipatikana atakuwa mwafaka zaidi.
Axel Witsel (Pauni 35 milioni)
Witsel alihamia Zenit mwaka 2012 kwa dau la Pauni 32.5 milioni na tangu hapo hajasita kuelezea tamaa yake ya kucheza katika Ligi Kuu ya England.
Nyota huyu wa Ubelgiji kama akienda Manchester City ataungana na wakali wenzake kutoka nchi ya Ubelgiji kama vile Vincent Kompany na Dedryck Boyata.
Akiwa na umbo refu kama Toure, Witsel amefunga mabao 59 katika mechi 229 lakini amejulikana zaidi kutokana na kulimudu vyema jukumu lake la kiungo mkabaji.
Javi Martinez (Pauni 35 milioni)
Mhispaniola huyu ameonekana kupata wakati mgumu kujihakikishia nafasi ya kudumu Bayern Munich. Majeruhi yake yamemfanya Kocha Pep Guardiola kumnunua Xabi Alonso kutoka Real Madrid.

No comments