Namna ya kuwa mrembo baada ya kujifungua

KUPATA mtoto ni baraka kutoka kwa Mungu. Hata hivyo wanawake wengi waliokuwa warembo katika siku za nyuma hushindwa kuendeleza ubora wao baada ya kujifungua, hiyo ni kwa kuwa wanakuwa ‘bize’ na malezi. Makala haya yanaelekeza namna ya kuwa na mwonekano mzuri baada ya kujifungua.


Kwanza angalia kuna mitindo gani ya mavazi wakati huo. Kumbuka wakati ukiwa na mimba ulikuwa ukiangalia mitindo ya nguo pana ambazo zinaweza kukutosha kutokana na ukubwa wa mwili hasa maeneo ya tumboni. Ukifahamu mitindo mipya ya nguo jaribu kuvaa kisichana na utaonekana umependeza.

Kula chakula bora lakini epuka kula kupita kiasi. Kwa wale wanaonyonyesha ni vizuri kula chakula laini ambacho kina vitamini zote kwa ajili ya mtoto.

Jikite kwenye mazoezi ya mara kwa mara hususan yale ya kupunguza tumbo. Unatakiwa kufanya mazoezi hayo kwa miezi michache kwani kwa kawaida huwa ni kazi ngumu kumaliza tumbo. Tafuta krimu maalumu za kukuondolea mistari ya unene ‘stretch marks’ hasa maeneo ya tumbo na nyonga.

Usisahau kuupamba uso wako mara kwa mara kila unapopata nafasi. Kumbuka kuwa baada ya kujifungua maisha mengine yanaendelea.
Kwa kuwa utakuwa bize na malezi, pendelea kusuka mitindo mizuri ya nywele kila mara. Kumbuka kuwa itakuwa ni kazi kubwa kwenda saluni mara mbili kwa wiki kwa ajili ya kutengeneza nywele za kawaida.
Unaposhindwa kupata nafasi ya kwenda saluni mara kwa mara maana yake ni kwamba hutakuwa na mwonekano mzuri.

No comments