Msuva: Kuanzia benchi raha sana
Msuva aliingia kipindi cha pili kwenye mchezo huo akichukua nafasi ya Haruna Niyonzima na kufanikiwa kufunga mabao hayo na kuiwezesha Yanga kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya kikosi cha wachezaji 10 wa Mgambo
WINGA mwenye kasi zaidi kwenye kikosi cha Yanga, Simon Msuva, amesema chachu ya kuifunga Mgambo JKT mabao mawili juzi Jumamosi ni yeye kuanzia benchi kwani alipata muda mzuri wa kuwasoma wapinzani na kufahamu mapungufu yao.
Msuva aliingia kipindi cha pili kwenye mchezo huo akichukua nafasi ya Haruna Niyonzima na kufanikiwa kufunga mabao hayo na kuiwezesha Yanga kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya kikosi cha wachezaji 10 wa Mgambo.
Winga huyo alisema licha ya kwamba Yanga walifanikiwa kushinda, bado wapinzani wao walionekana kuwa wazuri na kuwapa changamoto kubwa.
“Nilipokuwa benchi nilifanikiwa kuwasoma wapinzani, nilifahamu uzuri wao na ubovu wao, hivyo nilivyoingia kazi yangu haikuwa ngumu sana,” alisema.
“Kocha pia alinipa maelekezo ya namna ya kwenda kupenya kwenye ukuta wa wapinzani wetu ambao walionekana kuwa imara sana, haikuwa kazi rahisi lakini nilijitahidi kupambana.
Post a Comment