Pacha wanaoshirikiana mwanamume, kazi, gari, kitanda

Pacha wanaofanana kwa kila kitu

Pacha waliozaliwa kwa kupishana dakika moja, wanashirikiana kila kitu maishani. Maisha ya kawaida, gari, akaunti ya facebook, benki, mshahara, kazi hata rafiki wa kiume, yote hayo wanafanya kwa kushirikiana.
Mabinti hao raia wa Australia, Anna na Lucy DeCinque (28), pia wanatumia kiasi kikubwa cha pesa kufanya upasuaji wa kuondoa kitu chochote kitakachowafanya wasifanane.
Wamefanya upasuaji wa kuongeza matiti katika kiwango kimoja ufanano wao ubaki kama ulivyo, wametengeneza midomo, kope za kwenye macho na mambo mengine mengi ya kulinda namna wanavyotaka kufanana.
Matumizi yao ya kukarabati mwili yamewagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 217,430 (Sh365.6 milioni).
Ni nadra sana pacha hawa kutembea kila mtu kwa wakati wake, muda wote wanakuwa pamoja, wanalala muda mmoja, wanatumia gari moja na kitanda kimoja pia.
Pacha hawa wanaoishi katika mji wa Perth, Mashariki nchi ya Australia, bado wanaishi na mama yao anayeshuhudia namna mabinti zake wanavyopatana.
Ingawa kila mmoja ana utashi na vitu anavyopenda maishani, lakini wamechagua kuwa na rafiki wa kiume mmoja anayetoka nao wote kwa pamoja na wakati mmoja

No comments