Aunty Ezekiel: Jamani niacheni ni maisha yangu
Aunty Ezekiel
NYOTA wa filamu za Kibongo, Aunty Ezekiel amesema hapendelei kuwaona watu wakimsumbua kwa kumtaka afanye wanavyotaka wao, ilhali yeye ana maisha yake binafsi.
Mwigizaji huyo aliyefanya sherehe ya kuzaliwa siku
chache zilizopita, alisema licha ya kwamba yeye ni kioo cha jamii,
lakini kuna wakati anapaswa aachwe ili aishi maisha yake binafsi, kwani
anaamini umaarufu siyo mzigo.
“Nikiwa kama msanii ninapaswa kuishi maisha ya
aina fulani ili niwe mfano kwa jamii, kinachonishinda ni watu wanaotaka
niishi vile wanavyotaka wao, jambo ambalo si sahihi, ni vizuri
wakakumbuka kwamba na mimi ni binadamu na nina maisha yangu binafsi,”
alisema na kuongeza:
“Mfano katika akaunti zangu za mitandao ya
kijamii, watu wananichagulia picha za ‘kupost’ kila siku kioo kioo,
mnatuita vioo vya jamii wakati mnatutukana kila siku, kioo changu
kimevunjika mjue hivyo nitafanya vile ninavyotaka na si mtakavyo ninyi,”
alijigamba mwigizaji huyo.
Post a Comment