WASHIRIKI MISS TANZANIA 2014 WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA MIKUMI
Warembo
wanaoshiriki shindano la Redd's Miss Tanzania 2014 wakipozi jirani na
bwawa la viboko na mamba lililopo katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi
wakati warembo hao walipotembelea hifadhi hiyo jana ikiwa ni sehemu ya
kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Mwongoza
watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro, Benina
Mwananzila akiwapa maelezo warembo wa Redd's Miss Tanzania 2014 juu ya
bwawa la viboko na mamba lililopo katika hifadhi hiyo wakati warembo hao
walipotembelea hifadhi hiyo jana ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii
wa ndani nchini.
Mwongoza
watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro, Ibrahim
Kassim akiwapa maelezo warembo wa Redd's Miss Tanzania 2014 juu ya sifa
kuu za hifadhi wakati warembo hao walipotembelea hifadhi hiyo jana ikiwa
ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Kaimu Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Mikumi mkoani Morogoro, Apaikunda Mungure akiwagawia vipeperushi vilivyo na taarifa mbalimbali za hifadhi hiyo warembo wa Redd's Miss Tanzania 2014 waliotembelea hifadhi hiyo jana ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani.
Warembo
wa Redd’s Miss Tanzania 2014 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada
ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa Mikumi jana ikiwa ni sehemu ya
kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Warembo
wa Redd’s Miss Tanzania 2014 wakiwa Camp ya Mbuyu iliyopo katika
Hifadhi ya Taifa Mikumi jana walipotembelea hifadhi hiyo ikiwa ni sehemu
ya kuhamasisha utalii wa ndani nchini.
Post a Comment