Mauzo ya jezi za Jaja ni kufuru Morogoro

WAKAZI wa Morogoro nao wameingia kwenye
presha kubwa ya Ligi Kuu Bara lakini zaidi ni
kuhusu straika mpya wa Yanga, Geilson
Santos ‘ Jaja’ ambaye jana alikuwa kivutio
kwenye mazoezi ya timu yake katika Uwanja
wa Jamhuri , Morogoro.
Jaja alikuwa kivutio na kusababisha uwanja
huo kujaa watu kama vile wameenda
kutazama mechi , kuona hivyo Wanayanga
wengi wakasema : “Lazima tuwachinje hao
Mtibwa .”
Straika huyo raia wa Brazil alikuwa kivutio
kiasi cha kusababisha mauzo ya jezi za
Yanga zenye jina lake mgongoni kuwa
makubwa, huku umati ambao ulijaa uwanjani
hapo kwa kiingilio cha shilingi 500 ukizinunua
jezi hizo kwa wingi kwa kitita cha kuanzia Sh
15, 000 hadi 10, 000.
Ikiwa chini ya kocha wake , Marcio Maximo ,
Yanga ilifanya mazoezi mepesi kwa dakika
sitini kisha kuingia kwenye basi lao na
kuondoka uwanjani hapo .
Licha ya kuondoka, bado idadi kubwa ya
mashabiki iliendelea kumiminika na kutoamini
kama kweli Yanga wameondoka. Timu hiyo
ipo mkoani hapa kwa ajili ya kukipiga na
Mtibwa Sugar katika mechi ya Ligi Kuu Bara,
leo Jumamosi .

No comments