Unajua maana ya pete ya uchumba ? Soma hii

MARRIED BUT NOT ENGAGED
Hivi unajua maana ya neno
“ engagement ?” yaani kile kitendo cha
mwanaume kutangaza mbele ya umma
jinsi moyo wake ulivyompenda binti
fulani na kama alama ya kuthibitisha
nia hii ya dhati kijana huyu anachukua
pete na mumvika binti huyu .
Kama ni kwa wenzetu wazungu basi
kijana atapiga goti na kumuuliza
mwanadada “ will you marry me ?” Mara
baada ya tendo hili hakuna kijana
yeyote anayeweza kuja kutangaza
kumpenda binti huyu , na kinachofuta
hapo ni mipango ya ndoa .
Neno “ engagement ” linatokana na neno
“ engage ” , neno “ engage ” humaanisha
kuchukua nafasi “ to occupy ” ,
kujihusisha kwa dhati au kuamua
kuhusiana kwa dhati “ to involve ” au pia
“ to absorb” .
Maneno haya yote ya kiingereza
yanamaanisha kwamba mara kijana
anapoamua kum “ engage ” mpenzi wake
wakike wote wawili wame kubali
kumilikiana , kila mmoja kushukua
nafasi kubwa kwenye moyo wa
mwenzake , kila mmoja kuumeza moyo
wa mwenzake kwa penzi , na pia kila
mmoja kuamua kwa dhati kujihusisha
vilivyo katika maisha ya mwenzake .
Sasa kama hizi ndizo maana za kile
kitendo ulichomfanyia mke wako miaka
hiyo ya nyuma au kama hii ndiyo
maana ya kile ulichofanyiwa na mumeo
siku zile akikuchumbia , nikuulize , je
maana ile ya “ engagement” bado ni
halisi hadi leo???? Au iliishia siku ile ile
ya “ engagement ?” au yamkini ulivikwa
tu pete na ukafurahia pete ambayo ni
alama tu wakati kamwe hujawahi
kuuona upendo ambao pete hiyo
iliumaanisha?
Na je , kwa kutazama maana hizi
nilizozitoa , ukiangalia mahusiano yenu
unaona ile “ engagement ” bado ipo???
Au ilishakufa ??? Au haijawahi
kuwapo?? Kama jibu ni ilishakufa au
haijawahi kuwapo basi hiyo pete ya
“ engagement ” kidoleni kwako ni mzigo
tu, kwanza unaweza kukuta hata aliye
ku “ engage ” haishi na wewe tena, ana
wengine , sasa hiyo alama
inamuwakilisha nani hapo kidoleni ?
Kama unapete ya “ engagement ”
kidoleni jiulize , Je hii ni alama ya
ushuhuda wa penzi halisi katika
mahusiano yetu ? Au ni alama ya
kihistoria inayoonyesha kitu ambacho
hakipo tena? Kama ni alama ya
kihistoria basi haistahili kuwa kidoleni
bali kwenye nyumba ya makumbusho
“ take it to museums”
By Remmy B.M

No comments