MAMBO AMBAYO WANAUME WENGI HUZINGATIA WAKATI WA KUFANYA MAAMUZI YA KUOA

Wanaume wengi wanapofikia hatua ya
kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa
mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali
huchukua muda wao mwingi kuchunguza
mambo mengi juu ya wake ambao
wanadhani kwamba wanaweza kuwa
pamoja kwa kipindi chote cha maisha .
Wanawake wengi wanajisahau na kudhani
kwamba kitu kinachoweza kuwafanya
wakapata wachumba ni uzuri hivyo
kupoteza muda wao kujichubua na
kujiremba ili wawavutie wanaume bila
kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.
Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na
kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura
nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia
100 za kuolewa . Utafiti ambao nimeufanya
unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia
na umbo, kuna kuna sifa nyingine za
msingi ambazo mwanamke anatakiwa
kuwa nazo ili aweze kuwa katika
mazingira mazuri ya kupata mchumba wa
kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo
ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea
mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa .
MWEYE MAPENZI YA KWELI
Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka
kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa
mwanamke na ikiwezekana waweze kupata
watotoa ambapo watoto mara ndio
wamekuwa furaha ya ndoa . Wapo
wanawake wengine ambao wanonesha wazi
kutokuwa na mapenzi ya kweli bali
wanakuwa na mapenzi ya kuzuga.
Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu
tu kwamba yuko na mtu fulani ama
kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume
lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati
kutoka moyoni mwake. Mwanamke asiye
na mapenzi ya dhati utamgundua tu , muda
mwingi utamuona macho yake yako
kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona
kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha
mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali
inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi
yanaanza kufifia .
Kwanini wanaume wanapenda wana wake
wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni
mwao na si kutokana na fedha walizonazo ?
Hii inatokana na ukweli kwamba maisha
siku zote yanabadilika , kama waswahili
wanavyosema , kuna kupanda na
kushuka .Sio kwamba kila siku utakuwa na
maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi
ushukuru mungu .Hivyo basi mwanamke
wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe
tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati
wakati wote wa maisha yao na si kwa
kipindi fulani tu cha neema .
Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha
ya ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa
hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana
kwa wanaume wengi kuiangalia ili wasije
wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye
baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo
hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi
maisha ya raha mustarehe .
WENYE TABIA NZURI
Tabia njema ndio silaha ya maisha , ukiwa
na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni
katika maisha ya kawaida. Lakini
linapokuja suala na kuoa tabia inakuwa
kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo
inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo
wasichana wazuri wenye mvuto wa aina
yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa
wanaume wa kuwaoa , ukiuliza kwani
utaambiwa anatabia mbaya. Naweza
kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa
kwa baadhi ya wanawake kukosa wanaume
wa kuwaona . Hakuna mwanaume hata
mmoja kati ya wale ambao nimejaribu
kuongea naye ambaye ameonesha
kulidharau suala hilo la tabia .
Si hivyo tu wapo wanaume ambao
wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa
kuangalia sura tu bila kujali tabia ,
matokeo yake baada ya siku chache
yanatokea machafuko ya aina yake hali
ambayo imepelekea kuvunjika kwa ndoa
kutokana na tabia mbaya alizonazo
mwanamke.
WENYE UCHU NA MAENDELEO
Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko
ya aina yake kwa wanaume , wengi sasa
hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke
ambaye hana kazi yaani 'golikipa '. Kama
atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa
maendeleo kwa kujituma kufanya kazi
mbalimbali za kimaendeleo kama vile
kilimo kwa wale walio vijijini na biashara
ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini
na hata vijijini . Ile dhana ya kusema
mwanamke ni mama wa nyumbani wa
kukaa na kujipodoa akimsubiria mwnaume
arudi amstarehesha , sasa hivi imepitwa na
wakati . Wanaume wengi wanapenda
wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye
ndoto za maendeleo katika maisha yao .
Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini
wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao
juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe .
WASIOPENDA MAKUU
Kuna wanawake wengine wanakuwa na
tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza
kuwa kero kwa wanaume . Wapo wanawake
ambao wanapenda makuu bila kujali hali
halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza
kusema wana tamaa , kila wikiendi
utamsikia " leo tunakwenda wapi dear ?"
Akimuona rafiki yake kanunua simu ya
laki tatu na yeye utamsikia akisema , ‘na
mimi naomba uninunulie simu kama ya
Grace ’. Ukienda naye Pub anakuambia,
" mimi sinywi pombe za chupa natumia za
kopo tena Heineken ’ . Yeye hajali kiasi cha
pesa mwanaume alicho nacho na
usipotekelezea anachukia na anaweza hata
kupunguza mapenzi.
Wanawake kama hawa wako katika
mazingira magumu sana ya kuweza kupata
wanaume wa kuwaoa . Mara nyingi katika
maisha fedha huzungumza, kama
mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha
itakuwa rahisi sana kwa mwanamke
kupata kila atakachopenda lakini si kwa
kumwambia mimi nataka kitu
fulani. Mwanaune mwenyewe utamsikia
akisema, ‘ unataka nikununulie simu ya
aina gani, au leo unataka twende wapi ?’
hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema ,
‘mimi nataka uninunulie simu kama ya
fulani ama leo nataka twende sehemu
fulani. ’
Wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia
wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote
ambacho watahitaji kama tu pesa
haitakuwa tatizo . Kitu ambacho
kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya
mwanamke kupenda mambo makubwa bila
kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.
Kuna wanawake wengine wao si wasemaji
kabisa, yeye anasubiri leo amemletea hiki,
anapokea na kushukuru , kesho akiambiwa
twende beach anakubali . Au wengine
wanasubiri mpaka waulizwe wanataka
nini, ndio wanasema .
Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama
una shida ya kitu fulani na unafahamu
kwamba ukimweleza mwenza wako
anaweza kukusaidia , hapana ! kama unaona
kwamba uwezekano wa kupata kile
ambacho unakihitaji upo mweleze kwa
utaratibu naamini atakuelewa na
kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi
wanaume wengi ni ile ya kulazimisha
ufanyiwe kitu fulani wakati inawezekana
uwezekano haupo .
WAVUMILIVU
Wapo wanawake ambao sio wavumilivu
kabisa katika maisha .Tunajua kwamba
maisha siku zote hayatabiriki , yanaweza
kutokea matatizo ya kiafya ama
kifedha .Huu ndio wakati wa kuona
uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke
anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu
na pindi matatizo yanapotokea anachukua
uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo
siyo mwanamke wa kuoa . Wangapi leo hii
huwatoroka waume zao pindi inapotea
kuumwa , kufilisika ama kupatwa na tatizo
lolote ambalo kwa namna moja ama
nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao
kutingishika ?
Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo
kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati
kama nilivyozungumza hapo awali .
Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni
lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa
tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote,
yawe ya raha ama ya starehe. Hawa ndio
wale ambao wanaume wengi wengependa
kuwa nao maishani mwao.
Licha ya kupenda kuoa wanawake amabo
wana tabia hizo nilizozitaja hapo juu ,
wanachukizwa sana na wanawake ambao
wanavijitabia vidogo vidogo ambavyo
kimsingi havikubaliki katka jamii. Tabia
hizo ni kama wambea , wasio wakweli na
wawazi, wasioridhika , wagumu kusamehe
na wapesi wa kuchukia , wagomvi na wenye
roho ya kwanini .
Utafiti huu umefanyikwa kwa baadhi ya
wanaume ambao wanatarajia kuoa
wanawake ambao wanaoishi katika
maeneo mbalimbali jijini Dar - es - Salaam .
Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto
kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume
wanafurahi kuwa na wanawake wa aina
gani. Hata kama utakuwa umeshaolewa,
kama kuna wakati kunakuwa na
kutokuelewana baina yenu, chunguza
yawezekana kwamba unakosa mojawapo
ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu.
Waweza kubadilika kwani inawezekana

No comments