SIRI YA HERUFI YA MWANZO YA JINA LAKO

HERUFI A
Mwenye jina linaloanziana na herufi A
ni mtu anayependa mambo makubwa,
anajiamini na mwenye uwezo wa
kutimiza malengo yake . Ni mtu mwenye
tahadhari, mchangamfu na mpenda
matukio . Anapenda Kuheshimiwa ,
anapenda Mamlaka , na ana kiburi , na
hasira .
HERUFI B
wenye jina linaloanziana na herufi B ni
mtu, mkarimu , muaminifu, na hupenda
kazi. Ni Jasiri , shujaa na mkatili katika
vita au pale anapotaka kulinda vilivyo
katika himaya yake .
HERUFI C
Mwenye jina linaloanziana na herufi C
ni mtu wa kukubadilika badilika ,
mshindani na hupenda kupigania
malengo yao wanayopenda . Ni watu wa
wabunifu na wanaopenda mawasiliano .
HERUFI D
Mwenye jina linaloanziana na herufi D
ni mtu anayependa usawa , Biashara. Ni
watu wanaopenda kuamrisha na
mwenye kupenda usafi . Ni jeuri na
wenye msimamo.
HERUFI E
Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni
mtu mwenye roho nzuri , yenye mapenzi
na huruma . mwenye kupenda uhuru
katika mapenzi na mchangamfu .
Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu
asiotegemewa na kigeugeu.
HERUFI F
Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni
mtu mwenye mapenzi , huruma , roho
nzuri na ana uwezo wa kuwafariji
watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye
huzuni lakini ni mzito wa kufanya
maamuzi.
HERUFI G
mwenye jina linaloanzia na herufi G ni
mtu mwenye mwenye imani ya kidini
na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha
kubuni na uwezo wa kutatua matatizo
ya watu . ni mtu mwenye hisia
kali, msomi, mpweke na mkaidi wa
kukubali ushauri wa kutoka kwa watu.
HERUFI H
Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni
mtu mwenye ubunifu na nguvu katika
biashara, hupata faida kubwa kutokana
na jitihada na bidii zake . ni mwenye
mawazo mengi , mchoyo na mbinafsi .
HERUFI I
Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni
mtu mwenye kupenda sheria , ana
huruma na utu . Wakati mwingi
hajiamini na ni mwenye hasira za
haraka .
HERUFI J
Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni
mtu mwenye matamanio ,mkweli,
mkarimu na muerevu. asiyekubali
kushindwa na hupata mafanikio
makubwa. Wakati mwingine anakuwa
ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo .
HERUFI K
Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni
mtu mwenye jeuri . mwenye msimamo
thabiti, mashuhuri na mwenye uwezo
wa kushawishi na kuamsha hisia za
watu wana uwezo wa utambuzi ambao
watu wengi hawana . ni mtu asioridhika
na hali ya kimaisha .
HERUFI L
Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni
mtu wa vitendo, mwenye hisani na
aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa
wanapata ajali mara kwa mara .
HERUFI M
Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni
mtu mwenye kujiamini sana,
mchapakazi na hupata mafanikio . ni
mtu mropokaji ,mwenye haraka na
mwepesi kukasirika .
HERUFI N
Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni
mtu mwenye ubunifu, hisia kali na
hupenda kuwasiliana lakini ana wivu
sana.
HERUFI O
Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni
mtu mwenye subra , mvumilivu na
mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu
mwenye kupenda kutumikia jamii na
mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti
hisia .
HERUFI P
Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni
mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na
hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho
lakini anapenda sana kujitumbukiza
kwenye mambo ya watu.
HERUFI Q
Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni
mtu mwenye kupenda mambo ya asili.
Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo
wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata
hivyo ni mtu aliyepooza sana.
HERUFI R
Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni
mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma
lakini ana hasira za haraka . Muda wote
anakuwa mpenda amani.
HERUFI S
Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni
mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta
utajiri . Ni watu wenye maamuzi ya
ghafla na hupenda mageuzi makubwa.
HERUFI T
Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni
mtu mwenye kupenda ushauri wa
kiroho, anatumia nguvu za ziada
kusaidia watu na hupata mafanikio
baada ya muda mrefu. Ni watu wenye
hisia kali sana na ni wepesi
kushawishika .
HERUFI U
Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni
mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla .
Anapenda uhuru katika mapenzi .
Lakini ni mtu mbinafsi , mwenye tamaa
na aliyekosa maamuzi.
HERUFI V
Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni
mtu Mchapakazi , wenye bidii na asie
choka. Hata hivyo ni watu
wasiotabirika .
HERUFI W
Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni
mtu muwazi , wachangamfuu kupita
kiasi na mwenye uwezo wa kutambua
mtu mwema na mbaya . Ni watu wenye
tamaa na hufanya mambo ya hatari.
HERUFI X
Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni
mtu asiyependa kuwekewa vizuizi
katika kwenye anasa na ni rahisi
kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa
uaminifu.
HERUFI Y
Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni
mtu mwenye kupenda Uhuru na
hawapendi kupingwa jambo lao lolote.
Ni watu wanaokosa uamuzi na
husababishia kupoteza bahati katika
maisha .
HERUFI Z
Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni
mtu mwenye kupenda matumaini na
amani. Ni wenye msimamo mkali ila
wanashauriwa kufikiria kabla ya
kuamua jambo
Mimi herufi ya jina langu imeendana
na maelezo hapo juu, wewe je. . . . . !!!!???

No comments