Simba yamzuia Coutinho ... kucheza ligi kuu
ZIKIWA zimesalia wiki tatu kabla ya mechi ya
watani wa jadi ambao wana jina kubwa
katika soka la Tanzania , Simba na Yanga
kukutana kwenye Ligi Kuu Bara, kumeibuka
mazito juu ya kiungo mshambuliaji wa
Yanga, Andrey Coutinho.
Habari ambazo zimefika kwenye meza ya
gazeti hili ni kuwa , baadhi ya mashabiki wa
Yanga wanataka Mbrazili huyo aendelee
kuwa nje mpaka siku ya mechi ya Simba,
Oktoba 12 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar .
Coutinho kwa sasa ni majeruhi ,
anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha
mguu na ataukosa mchezo wa leo dhidi ya
Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri ,
Morogoro. Utashi huo wa Wanayanga hao
maana yake ni kuwa , anatakiwa akose mechi
tatu ili akiivaa Simba awe fiti .
Kabla ya kuivaa Simba, Yanga itakutana na
Mtibwa , Tanzania Prisons ( Septemba 28 ) na
JKT Ruvu ( Oktoba 5 ) , wakati Simba itakipiga
dhidi ya Coastal , kesho Jumapili , Polisi
Morogoro ( Septemba 27 ) na Stand United
( Oktoba 4) .
Chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi
wa Yanga, kimesema kuwa wanachama
wameshazungumza na uongozi wao japo siyo
rasmi , lengo kubwa ni kukwepa mchezaji
huyo kujitonesha katika mechi hizo za hapo
kati hivyo kuikosa Simba. “Hawataki Coutinho
aikose Simba kabisa , suala hilo kwao
halitakiwi , tayari wameshaona kazi ya Jaja
katika Ngao ya Jamii dhidi ya Azam .
“Unajua viwanja vingi vya Bongo hasa hivyo
vya mikoani ni majanga , Coutinho
apumzishwe tu hizo mechi tatu ili akiivaa
Simba awe fiti na waione shughuli yake , ”
kilisema chanzo hicho na kuongeza :
“Pia kuna mabeki ambao wanaweza
kumpania na kumuumiza ili wamuumize kwa
makusudi, kiukweli kabisa msimu huu
hatutaki kufungwa wala sare zaidi ya ushindi
kila tutakapokutana nao .”
Kiungo huyo hakujumuishwa kwenye msafara
wa wachezaji walioenda Morogoro kutokana
na kuwa majeruhi . Juzi , Championi Jumamosi
lilimshuhudia mchezaji huyo akifanya
mazoezi ya kukimbia na kuuchezea mpira tu
huku akiwekwa kando kujumuika na wenzake ,
hali ambayo inaonyesha bado hajawa fiti
licha ya kuwa daktari wa Yanga, Juma
Sufiani hakuwa tayari kulizungumzia suala la
mchezaji huyo.
Post a Comment