Cannavaro awaonya Yondani , Twite Yanga

NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub
‘ Cannavaro’ , amewataka walinzi wenzake na
wachezaji kwa ujumla kucheza kwa umakini
mkubwa na kutoruhusu kufungwa mabao ili
waweke rekodi mpya.
Katika rekodi za Ligi Kuu Bara, hakuna hata
timu moja iliyomaliza ligi hiyo bila ya
kuruhusu bao hata moja na badala yake
Simba na Azam pekee ziliwahi kumaliza
msimu wa ligi bila ya kupoteza mchezo hata
mmoja .
Safu ya ulinzi ya Yanga inayounda kikosi cha
kwanza ni Cannavaro, Kelvin Yondani, Oscar
Joshua na Juma Abdul huku langoni akiwa
Deogratius Munishi ‘ Dida’ na ilifanikiwa
kutoruhusu bao katika ushindi wa mabao 3 -0
kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya
Azam .
Katika msimu uliopita wa ligi , Yanga iliweza
kuruhusu kufungwa mabao 19 ambapo
walimaliza ligi wakiwa nafasi ya pili nyuma
ya mabingwa , Azam FC.
Akizumgumza na Championi Jumamosi ,
Cannavaro alisema kuwa wameanza katika
mchezo wa Ngao ya Jamii na makali hayo
watayahamishia kwenye ligi kwa kuanza na
Mtibwa Sugar leo katika Uwanja wa Jamhuri ,
Morogoro.
“Mimi na wenzangu tumejipanga kuhakikisha
nyavu zetu hazitikiswi kwenye michezo ya
ligi kwani safu yetu ya ulinzi iko imara zaidi
ya msimu uliopita na kwa kuwadhihirishia
mashabiki basi waje kwa wingi kuona
tutakapocheza mchezo wa kwanza wa ligi
dhidi ya Mtibwa , ” alisema Cannavaro

No comments