Sababu za kufukuzwa kazi Rais wa shirikisho la muziki Tanzania

Hii
ni moja ya habari kubwa za Magazeti ya
leo Tanzania ambapo gazeti la Uhuru
limeandika kwamba Rais wa shirikisho
la muziki Tanzania Addo Novemba
amefutwa kazi baada ya kuhusika na
upotevu wa pesa za rambirambi ya
Mwanamuziki.
Zilikua ni pesa zilizotolewa kama
rambirambi kwenye msiba wa
Mwanamuziki wa siku nyingi Tanzania
mzee Gurumo ambazo zilikua ni milioni
1.1.
Fedha hizo zilikua zitumike kumnunulia
Bajaji mke wa Marehemu Pili Kitwana
lakini ikashindikana ambapo sasa nafasi
hiyo ya Rais inashikiliwa na Stara
Thomas kwa muda.
Addo Novemba alivuliwa madaraka hayo
mwezi uliopita lakini alipinga uamuzi
huo akidai ni batili lakini sasa Katibu wa
shirikisho hilo amesema Wanachama
wameridhia kumng’oa kwa sababu
ameichafua TMA.

No comments