Mwanamke Abakwa , Anyongwa kisha atupwa kichakani huko Mkuranga

MKAZI wa Kijiji cha Bupu kata ya Bupu
Tarafa ya Mkamba wilaya ya Mkuranga
mkoani Pwani Forodesi Ntabegera (30)
ameuwawa kwa kubakwa kisha
kunyongwa na watu wasiojulikana kisha
mwili wake kutupwa kichakani.
Kwa mujibu wa taarifa ziliotolewa na
kaimu kamanda wa polisi mkoani Pwani
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo
Mrakibu Msaidizi wa Polisi (SSP)
Athuman Mwambalaswa Marehemu
kuwa marehemu alinyongwa na watu
hao kwa kutumia kitenge chake
alichokuwa amekivaa.
Kamanda Mwambalaswa alisema kuwa
tukio hilo lilitokea Septemba 9 mwaka
huu majira ya saa 8:00 mchana baada
ya wakazi wa kijiji hicho kufanya msako
wa kumtafuta marehemu ambaye
alipotea Septemba 8.
“Baada ya msako huo kufanyika mwili
wa marehemu ulikutwa kwenye kichaka
umbali wa mita 30 kutoka barabarani
ambapo mwili wake ulimwagiwa unga
sehemu za kichwani na mgongoni,”
alisema Kamanda Mwambalaswa.
Alisema watu hao walitumia mfuko wa
salfeti aliokuwa amebebea unga aliotoka
kuusaga mashine, kumvisha miguuni
kisha mwili wake waliulaza kifudifudi.
Aidha alisema kuwa taarifa za kupotea
marehemu zilitolewa na kituo cha polisi
Kimazinchana na mwenyekiti wa Kijiji
cha Bupu Kasimu Kambangwa
walioongozana na watoto wa marehemu
ambao walidai mama yao alitoweka
baada ya kuaga kuwa anakwenda kusaga
na hakuonekana tena hadi mwili wake
ulipokutwa kwenye eneo hilo.

No comments