Diva Afunguka tena … Adai Zitto Kabwe ni mume wake na anatambulika kisheria

Mtangazajiwa Kipindi cha Ala za Roho
kinachorushwa kupitia Radio Clouds FM
ya jijini Dar, Loveness Malinzi ‘Diva’
kwa mara ya kwanza, amejilipua
kuzungumzia uhusiano wake na Zitto
Kabwe kwamba walikuwa mke na
mume.
Katika mahojiano maalum na
mwanahabari wetu jijini Dar juzi, Diva
alisema anashangazwa na baadhi ya
vyombo vya habari kumnyima uhuru
wa kuongelea suala lake na ‘zilipendwa’
wake huyo wakati kisheria yeye ni mke
wake hivyo anapaswa kuzungumzia
kutengana kwao.
“Ninyi mnayaongelea mambo ya Zitto na
mimi juu kwa juu tu hamjui kama mimi
nimeishi naye kama mke na mume
nyumbani kwake Masaki (Dar), sasa nini
kilisababisha penzi letu kuvunjika watu
hawajui, nina ushahidi wa kutosha lakini
wanaongeaongea tu,” alisema
Diva.Akaongeza:
“Sasa ninavyojua mimi kwa sheria za nchi,
mwanamke na mwanaume wakiishi pamoja
kwa zaidi ya miezi sita tayari ni mke na
mume. Hawezi kuniacha kirahisirahisi tu.”
Diva alikwenda mbele zaidi kufuatia
kauli ya Zitto aliyoitoa hivi karibuni
kupitia Kipindi cha Mkasi
kinachorushwa hewani na Runinga ya
East African Television ‘EATV’ na
mtangazaji Salama Jabir.
Zitto aliulizwa ana uhusiano gani na
Diva, naye akajibu ni mtu
wanayefahamiana tu lakini si mpenzi
wake.
Ilidaiwa kwamba, majibu hayo ya Zitto
kwa Salama ndiyo yaliyoibua hasira ya
Diva hadi kufikia hatua ya kutupia
kwenye ukurasa wake wa Instagram, e-
mail aliyodai aliwahi kutumiwa na Zitto
siku za nyuma akimtaka asiwe anaweka
wazi uhusiano wao kwa sababu
atachafuka kisiasa.
Diva
E-mail ilisomeka hivi:
“Unanikosea sana ujue unapoweka
mambo yetu hadharani. Ninaonekana
siwezi kuwa kiongozi kwa sababu
nashindwa ku-handle masuala yangu
binafsi.
“Madhara uliyoyafanya ni makubwa
sana. Wapinzani wangu wa kisiasa
watayatumia sana dhidi yangu.
“Ungekuwa unajua madhara yake
usingethubutu kufanya ulivyofanya mara
tatu sasa. Sijui nia yako nini, ila ipo siku
utajua umenikosea sanasana.”
Swali la mwandishi:
Je, Zitto akikubali kufuata huo utaratibu
uwe mkewe utamuacha GK ambaye
umekuwa ukimtangaza kuwa mpenzi
wako?
Diva: Hilo nitakujibu baadaye.
Siku za karibuni, baadhi ya vyombo vya
habari vimekuwa vikiripoti uhusiano wa
Diva na Zitto bila kuzama kwa undani.
Kufuatia Diva kutupia madai hayo
mtandaoni na kudai yeye ana hadhi ya
mke kwa Zitto na kauli ya Zitto kwenye
runinga kwamba Diva si mpenzi wake,
baadhi ya watu waliozungumza na
Amani walionesha kwenda kinyume na
mtangazaji huyo.
Wengi walidai kwamba wana
kumbukumbu zilizonyooka kwamba
Diva amewahi kujinadi kutoka na
Mbongo Fleva, Gwamaka Kaihula ‘Crazy
GK’.
“Sasa Diva anavyodai ni kama mke wa
Zitto mbona anamtangaza mwanaume
mwingine?” Alisema mkazi mmoja wa jiji
aitwaye Yuda.
Naye Ismail Juma, mkazi wa Kigogo, Dar
alisema aliwahi kusoma kwenye vyombo
vya habari kwamba Diva anapumzika na
mwanamuziki kutoka Kenya, Jackson
Makini ‘Prezzo’ kiasi cha kumzalishia
bifu na demu wa jamaa huyo, Huddah
Monroe.
“Diva awe na aibu basi, asikurupuke
wakati yeye mwenyewe si msafi kivile,”
alisema Ismail.
Kufuatia madai hayo, kwa muda wa siku
saba, Amani limekuwa likimsaka Zitto
kwa njia ya simu lakini bila
mafanikio.Watu wa karibu naye
walipoulizwa alipo, walisema
wanachojua ana shughuli zake nchini
Zambia.

No comments