Obama:'Ebola ni tisho kwa usalama


Rais Barack amezitaka nchi zengine kutoa
msaada wao katika kupambana na Ebola
Rais wa Marekani Barack Obama, amelitaja
janga la Ebola katika kanda ya Afrika Magharibi
kuwa tisho la usalama wa kimataifa.
Obama ametoa kauli hiyo huku akitangaza
jukumu la Marekani katika kupambana na janga
la Ebola.
''Dunia nzima inaelekeza macho ya kutaka
msaada kwa Marekani,'' alisema Rais Obama,
lakini akaongeza kwamba mlipuko
unaoshuhudiwa wa janga hilo, unahitaji
kushughulikiwa na jamii ya kimataifa.
Hatua ambazo Marekani imetangaza ikiwemo
kupeleka wanajeshi 3,000 katika kanda hiyo
kupambana na Ebola na kujenga taasisi za afya.
Ugonjwa wa Ebola umewaua watu 2,461 mwaka
huu, kulingana na shirika la afya duniani (WHO).
Utafiti wa chanjo ya Ebola
Tangazo hilo limetolewa huku Maafisa wa Umoja
wa Mataifa wakitaja ugonjwa huo kuwa janga la
kimataifa na pia janga kubwa kushuhudiwa
kwatika miaka ya hivio karibuni.
Pesa za msaada zinazohitajika kupambana na
Ebola zimeongezeka mara kumi katika mwezi
mmoja uliopita na kwamba dola bilioni ndizo
zinahitajika kukabiliana na ugonjwa huo.
Hii ni kwa mujibu wa mratibu wa Umoja wa
Mataifa kuhusu Ebola.
Rais Obama amezitaka nchi zingine kuongeza
kasi ya kusaidia katika vita dhidi ya Ebola kwani
kukithiri na kuendelea kuenea kwa ugonjwa huo
kutasababisha changamoto za kiuchumi ,
kiusalama na kisiasa.

No comments