Askari polisi wajeruhiwa kwa mlipuko wa bomu

ASKARI watatu wa jeshi la Polisi wamelazwa
katika Hospitali ya Mkoa wa
Ruvuma ( Homso ) iliyopo mjini songea
Mkoani humo wakiwa wanapatiwa matibabu
ya majeraha ambayo waliyapata baada ya
kushambuliwa kwa kitu kinachodhaniwa kuwa
ni Bomu la kurushwa kwa mkono .
Tukio hilo limetokea September 16, 2014
majira ya saa moja na nusu jioni katika kata
ya Msufini karibu na daraja laMatarawe ,
wilayani Songea Mkoani Ruvuma ambapo
watu watatu wasiofahamika walitupa kitu
kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa
kwa mkono ambalo limetengenezwa kienyeji
na kuwajeruhi askari hao watatu waliokuwa
doria .
Askari hao waliojeruhiwa ni WP . 10399 PC
Felista aliyejeruhiwa mguu wa kulia kwenye
unyayo na pajani , G . 7351 PC Ramadhani
aliye jeruhiwa mguu wa kulia karibu na goti
na tumboni upande wa kulia na G . 5515 pc
John aliyepata majeraha katika mguu wa
kulia chini ya goti na jeraha dogo tumboni.
Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa
Ruvuma Dr. Daniel Malekela ameeleza kutoa
vipande vya bati na misumari katika
majeraha ya askari hao na mpaka sasa
wanaendelea na matibabu.
Alisema kufutia hali hiyo Jeshi la Polisi
mkoani Ruvuma linaendelea na
uchunguzi wa kina ili kuwakamata wahusika
wa tukio hilo kwa hatua zaidi za kisheria .
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe. Saidi
Mwambungu kasema amesikitishwa sana na
kitendohicho cha wahalifu kujeruhi askari
tena kwa makusudi na amesema serikali
kupitiavyombo vyake vya ulinzi na usalama
watahakikisha wanawasaka na kuwakamata

No comments