Kibarua kinachoikabili Liverpool

Gerrad ''tunakibarua kigumu kuinua viwango
vyetu''
Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard amekiri
kuwa timu hiyo inakazi ya ziada kufanya
ilikupunguza pengo la uwezo wao na timu za
bara Ulaya ilikushamiri barani huko.
Nahodha huyo aliyasema hayo baada ya kufunga
bao la ushindi katika mechi yao ya kwanza ya ligi
ya mabingwa barani ulaya tangu mwaka wa
2009.
Liverpool iliilaza Ludogorets 2-1. Mabingwa hao
wa mwaka wa 2005 walikuwa wametikisa wavu
wakwanza kupitia kwa Mario Balotelli katika
muda wa majeruhi ya kipindi cha pili kabla ya
furaha yao kukatizwa mara moja na mkwaju wa
Dani Abalo.
Hata hivyo nahodha huyo alikabidhiwa jukumu la
kuipelekea mbele timu yake kupitia kwa mkwaju
wa Penalti mwisho wa mechi hiyo.
Gerrad ''ilikuwa bayana hata ushindi huo
haukuwa na nguvu kama kawaida yetu''
''tulicheza na tukashinda lakini hivyo sivyo nilivyo
tarajia mimi ''
''Najua lazima tufanye kazi ya ziada''
Liverpool, sasa wanajukumu la kuizima FC Basel
katika mechi yao ijayo ilikuihakikishia nafasi nzuri
ya kusonga mbele katika mkondo wa pili.
Basel jana ilikiona chamtema kuni ilipoambulia
kichapo cha mabao 5-1 mikononi mwa mabingwa
watetezi Real Madrid.
Kocha Brendan Rodgers alikiri kuwa ni wazi
wanakazi ya ziada kufanya ilikuhakikisha
watafuzu kwa mkondo wa pili.

No comments