Mgosi apewa ‘ uchawi ’ wa kuimaliza Yanga leo

WAKATI pazia la Ligi Kuu Bara likifunguliwa
leo , mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Mussa
Hassan Mgosi , ametamba kuwa
amekabidhiwa ‘ uchawi ’ wa kuiangamiza
Yanga.
Yanga wanatarajiwa kuwa wageni wa Mtibwa
katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu
unaotarajiwa kupigwa leo Jumamosi kwenye
Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.Mchezo wa
leo baina ya timu hizo unatazamiwa kuwa
mgumu kutokana na Yanga kuwa na ‘ gundu ’
katika uwanja huo ambapo bado ‘ wanadaiwa ’
kipigo cha mabao 3-0 walichokipata uwanjani
hapo Septemba 12, 2012 .
Akizungumza na Championi Jumamosi ,
Mgosi alisema kuwa mazoezi waliyofanya
pamoja na nidhamu ndani ya kikosi chao,
ndiyo silaha ya wao kuibuka ‘ kidedea’ ,
ingawa alikiri kuwa mchezo utakuwa mgumu
na wenye upinzani wa aina yake.
“Mchezo wetu dhidi ya Yanga ninaamini
utakuwa mgumu kutokana na uzoefu na
ubora wa kikosi chao , nimejipanga , lazima
niwaue Yanga Jamhuri , unajua nilikuwa
ninapewa mbinu mbadala za ‘ kuwamaliza ’
kwa hiyo mashabiki waje kwa wingi kuona
vita ya Jaja na Mgosi.
“Lengo letu ni kuvuna pointi nyingi na
tutaanzia kwa Yanga, ” alisisitiza Mgosi
ambaye aliwahi kukipiga katika Klabu ya
Simba na DC Motema Pembe ya DR Congo

No comments