Mechi za kufuzu AFCON zaendelea.. Pata matokeo

Mechi za kutafuta tiketi za fainali za kombe la
mataifa ya Afrika mwakani huko Moroko ikiwa ni
hatua ya makundi ambapo Uganda imeutumia
vema uwanja wa nyumbani wa Nelson Mandela
kwa kuinyoa Guinea mabao 2 kwa 0
Sudan ikicheza ugenini mjini Pwe Nwah
imeambulia kipigo cha magoli mawili bila majibu
kutoka kwa Jamhuri ya Kongo.
Bafana Bafana ya Afrika kusini imebanwa
nyumbani na mabingwa watetezi Nigeria kwa
kushindwa kufungana wakati Malawi imeinyuka
Ethiopia 3-2 mjini Blantyre.
Kwenye kundi C Angola wakashindwa kutamba
nyumbani kwa kichapo cha mabao matatu kwa 0
kutoka kwa Burkina Faso huku Lesotho ikitoka
sare ya bao moja moja na Gabon
Sierra Leone ikawahuzunisha watu wake kwa
kuiacha Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
ichukue pointi zote tatu kwa ushindi wa mabao 2
kwa 0, kama ilivyokuwa kwa Togo iliyokubali
kipigo cha mabao matatu kwa mawili kutoka kwa
Ghana.
Mjini Praia…Cape Verde imeirarua Zambia 2 bila,
Tunisia wakaitandika Misri 1 bila, nayo Msumbiji
ikatoka sare ya 1- 1 na Niger

No comments