Yanga chereko tupu.. Ni moto wa kuotea mbali

KIKOSI cha Yanga SC kimetwaa Ngao ya
Jamii baada ya kuichapa timu ya Azam FC
mabao 3 -0 katika mechi iliyopigwa Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi punde .
Mabao ya Yanga yamefungwa na Geilson
Santos ' Jaja ' dakika ya 56 na 66 huku bao
la tatu likiwekwa kimiani na Simon Msuva
dakika ya 87 ya mchezo .

No comments