Liverpool yaua , Arsenal yachapwa Uefa


Mashindano ya kutafuta klabu bingwa ya bara la
ulaya katika mchezo wa soka ilianza jana huku
timu kadhaa zikishuka katika viwanja
mbalimbali ili kuanza kuzitafuta point tatu
muhimu.
Mabingwa watetezi Real Madrid iliialika FC Basel
katika uwanja wa Benabeu na kuanza vyema
mbio za kutetea taji hilo kwa kuwafunga
wapinzani wao kwa jumla ya mabao 5-1 huku
washambuliaji wake wote wakiweza kuzifumania
nyavu za wapinzani wao.
Katika viwanja vingine Liverpool imeutumia
vyema uwanja wake wa nyumbani na kuibuka na
ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Ludogorets Razgrad
na kushuhudia mwanzo mzuri wa mshambuliaji
Baloteli aliyefunga moja ya mabao hayo mawili.
Wenyeji Olympiakos ikaibuka na ushindi wa
mabao 3-2 dhidi ya Atletico Madrid, huku timu ya
Benfica ikizamishwa na wageni wao Zenit St.
Petersburg kwa mabao 2-0, wakati Monaco
ikishinda bao 1-0 dhidi ya Bayer Liverkusen.
Dortimund ikashinda mabao 2-0 dhidi ya Arsenal
na Galatasary ikatoka sare ya 1-1 dhidi ya
Anderlecht.
Ligi hiyo inaendelea leo hii wakati Chelsea
itacheza nyumbani dhidi ya FC Schalke 04,
Bayern Munich dhidi ya Manchester city, AS
Roma dhidi ya CSKA Moscow, Ajax dhidi ya PSG,
Barcelona dhidi ya Apoel FC, NK Mariborv dhidi
ya Sporting Lisbon wakati Athletic Bilbao dhidi ya
Shakta Donestik na FC Porto itacheza na BATE.

No comments