Mipango ya kuisambaratisha Kagera Sugar

Simba yaipania Kagera Sugar
Simba moja ya timu kubwa Tanzania imeanza vibaya msimu huu kwa kutoka sare mechi sita kati ya saba ilizocheza kabla ya mapumziko marefu


BAADA ya kukiboresha kikosi chake katika dirisha dogo la usajili kocha wa Simba, Patrick Phiri amesema pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar zitawapa uhakika wa ubingwa kabla ya kwenda mapumziko mengine.
Patrick Phiri ameiambia Goal itapendeza endapo watashinda mpambano huo utakaochezwa siku ya Boxing day Desemba 26, ili wachezaji wake waende mapumziko wakiwa hawana msongo wa mawazo kuhusu mwenendo wa timu yao.
"Kisaikolojia ni vizuri kushinda mchezo huo ili wachezaji watakapokwenda mapumziko waweze kufuaria vyema sikukuu ya mwaka mpya kabla ya kuanza tena kazi ya kupigania ubingwa wa Tanzania bara msimu huu,”amesema Phiri.
Simba moja ya timu kubwa Tanzania imeanza vibaya msimu huu kwa kutoka sare mechi sita kati ya saba ilizocheza kabla ya mapumziko marefu na kujikusanyia pointi tisa na kukalia nafasi ya saba.

No comments