
Simba imemuongezea Okwi mkataba mpya wa mwaka mmoja baada ya huo wa miezi sita kuelekea kumalizika
KLABU ya Simba imeshinda kesi yake iliyokuwa imeiripotisha makao makuu ya Shirikisho la soka duniani FIFA kuhusu pesa za kumuuza mshambuliaji wake Emmanuel Okwi kwenye klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia na sasa timu hiyo imetakiwa kuilipa Simba SC , Dola za kimarekani 300,000 na fidia kwa usumbufuGoal imefahamu.
Simba waliishitaki klabu hiyo kunako Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo CAS baada ya Watunisia hao kukataa kuwalipa pesa za uhamisho wa mhezaji Emanuel Okwi, alipouzwa kutoka Simba kwenda Etoile Du Sahel.
FIFA imeamuru Etoile kuwalipa Simba kiasi hicho ambacho ni zaidi ya Tsh. Milioni 500 za Kitanzania baada ya kupitia kesi hiyo na kubaini kwamba Wekundu hao wa Msimbazi wanahaki ya kulipwa pesa zao kutokana na biashara hiyo iliyofanyika kihalali.
Wakati kesi hiyo ikiendeshwa FIFA, ilitoa ruhusa Okwi atafute timu ya kuchezea ili asipoteze kiwango chake, ambapo alirudi Uganda kucheza katika klabu yake ya zamani SC Villa lakini hakuchukua muda akauzwa Yanga SC ya Jijini Dar es salaam, hata hivyo hakukaa sana aliamua kutimkia Simba na kupewa mkataba wa miezi 6 na wiki hii Simba imemuongezea mkataba mpya wa mwaka mmoja baada ya huo wa miezi sita kuelekea kumalizika
Post a Comment