Hawa ndio Viungo bora wachezeshaji Ligi Kuu duru la kwanza


Haruna Niyonzima
Wametengeneza nafasi nyingi za kufunga kwa washambuliaji kwenye klabu zao hali kadhalika wamekuwa wazuri kwenye kufumania nyavu

Mzunguko wa kwanza Ligi Kuu Bara umefikia tamati baada ya klabu zote 16  kucheza michezo 15 ya nyumbani na ya ugenini
Ulikuwa mwanzo mbaya kwa baadhi ya wachezaji  wazawa na wageni pia kilikuwa ni kipindi kizuri kwa nyota kadhaa kwani walikuwa na mwanzo mzuri tangu ufunguzi wa Ligi
Goal inakuletea viungo bora wa ushambuliaji Ligi Kuu baada ya duru la kwanza
Kiungo mshambuliaji  huyu wa klabu ya Simba amekuwa na kiwango kikubwa chini ya mwalimu Joseph Omog, Muzamiru Yasin aliye ichezea Mtibwa Sugar kwa msimu uliopita tayari  amefunga magoli 4 na kutengeneza nafasi nyingi za magoli kwa washambuliaji wake pia  amekuwa ni mchezaji wa kudumu kwenye kikosi cha Mnyama tangu mwanzo mwa msimu
Ndiye silaha kubwa  kwa Wagonga Nyundo wa Mbeya mzunguko wa kwanza kwenye upande wa ufungaji , kiungo huyu amekuwa akicheza kwenye maeneo tofauti tofauti lakini amekuwa hatari sana hasa akichezeshwa eneo la kiungo mchezeshaji sifa kubwa ni uwezo wake wa kumiliki mpira michezo 15 ya duru la kwanza amefunga magoli 4
Licha ya kutopata nafasi kwenye michezo ya awali ila Mrwanda huyu amekuwa kivutio na msaada mkubwa kwenye kikosi chakecha Yanga  kwenye michezo ya mwishoni, Niyonzima maarufu kama Fabregas amekuwa akitengeneza mipango ya mashambulizi yote ya Wana jangwani  na amekuwa msaada mkubwa kwenye kurudisha  kiwango cha Msuva kwani amekuwa akimtengenezea nafasi nyingi uwanjani
Alianza kutumika kama mbadala wa mshambuliaji Ajibu ndani ya kikosi cha Mnyama Simba ila juhudi zake zimemfanya kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza, kiungo huyu mshambuliaji amefunga magoli 2 na kutengeneza magoli zaidi ya manne katika mechi 15 sifa yake kubwa ni mzuri kwenye kusoma madhaifu ya mpinzani

No comments