Hizi ni Vita 7 ndani ya Yanga

YANGA inatafuta kikosi chake cha kwanza kwa sasa wakati huu inapokaribia michuano ya Kombe la Kagame, hatua hiyo inakuja kufuatia usajili ambao timu hiyo imeufanya katika dirisha hili la usajili.
Wakati kazi hiyo ikiendelea tayari kuna vita vya chini chini kwa wachezaji katika kuwania nafasi imeanza kujitokeza ambapo wako wanaonyesha watapoteza nafasi zao kama ambavyo walivyojituma katika msimu uliopita, lakini pia wapo wapya ambao wanahitaji kuonyesha uwezo kuchukua nafasi katika kikosi cha makocha Hans Pluijm na Boniface Mkwasa.
Chini ni orodha ya vita saba vinavyopiganwa chini kwa chini baina ya wachezaji katika kusaka heshima mbele ya makocha wao kabla ya kuanza kwa Kombe la Kagame na msimu mpya wa ligi.
Mwinyi/Joshua
Wote hawa wanacheza beki ya kushoto, katika mchezo uliopita kati ya Yanga na KMKM ulikuwa ni jibu tosha kuna ingizo jipya Mwinyi Haji Mngwali ambaye ataingia vitani kugombea namba na Oscar Joshua ‘OJ’, lakini tayari Mwinyi ameanza kuonyesha mambo tofauti na Joshua.
Beki huyu aliyesajiliwa kutoka KMKM anaonekana kuwa imara kwa kupandisha mashambulizi na hata kushambulia kwa kupiga mashuti makali yenye maana kitu ambacho Joshua anapungukiwa kidogo hasa katika maamuzi ya mwisho juu ya afanye nini anapokuwa anapanda mbele.
Wakati ubora wa Mwinyi ukiwa hivyo Joshua naye ana ubora wake katika ukabaji hataki masihara Mwinyi kidogo anatakiwa kujifunza katika hili kwa mkongwe huyu, ingawa wengi tayari wanaona kuwa, nafasi ya Joshua katika kikosi cha kwanza kwa sasa mbele ya dogo hili la Kizenji ni ndogo.
Zuttah/Abdul
Mabeki wa kulia hawa Juma Abdul alikuwepo katika msimu uliopita na akafanya kazi kubwa kiasi cha wadau kupendekeza kwamba alistahili kuwepo katika kikosi cha Taifa Stars, lakini Yanga ikaona haitoshi ikamleta Mghana Joseph Zuttah katika nafasi hiyo.
Hakuna mtu ndani ya Yanga atasahau ubora wa Abdul katika msimu uliopita alifanya kazi safi ya kukaba na kupandisha mashambulizi, lakini kuna muda anapungukiwa na ubora zaidi katika kurudi kukaba wakati amepanda kushambulia anahitaji kupambana na Zuttah ambaye bado hajaonyesha kuwa imara zaidi.
Zuttah ni mzuri katika kupiga krosi lakini katika mchezo uliopita uliokuwa wa kwanza kwake ndani ya Yanga hakuwa imara katika kukaba, ingawa alionekana kwamba anaweza hata kucheza kama kiungo hasa juu ya maamuzi ake ya kupiga pasi za haraka na kuwapunguza wapinzani. Pia kuna muda kama anajisahau kidogo akichelewa kufanya maamuzi.
Ngoma/Tambwe

No comments