Hii ndio Simba aisee.. Kwa hizi plan mtakaa tu!

SIMBA iliweka kambi ya wiki mbili wilayani Lushoto, Tanga na kufanya mazoezi ya viungo, utimamu wa mwili na soka kidogo ili kuwarejesha nyota wake katika hali ya mchezo baada ya mapumziko ya mwisho wa ligi kwa muda mrefu.
Mara baada ya mazoezi hayo jeshi zima la Simba lilitua Dar es Salaam Ijumaa jioni na Jumamosi lilikwenda kuitazama Yanga ikicheza mechi ya ufunguzi ya Kombe la Kagame dhidi ya Gor Mahia ya Kenya na kukubali kipigo cha 2-1.
Kambi hiyo ya Lushoto na kitendo cha kocha mkuu wa Simba, Dylan Kerr, kocha wa viungo, Dusan Momcilovic na kocha wa makipa, Idd Salim kwenda kuitazama Yanga ilipocheza na Gor Mahia ni kama kuwazuga watani wao hao kwani Simba mpaka sasa hawajajifunza mbinu zozote za mchezo na ndiyo kitu wanachokwenda kukifanya katika kambi yao ya Zanzibar.
Kambi ya Lushoto ilidhamiria kuwajenga wachezaji kuwa fiti ili Kerr atakapoanza kuwapa mbinu wawe hodari na kuweza kuwapiku wapinzani wao Yanga ambao wameanza michuano ya Kagame kwa mwendo wa kusuasua.
Simba inaondoka leo Jumanne kwenda Unguja, Zanzibar kwa kambi ya wiki mbili ikiwa ni mwendelezo wa kambi yao iliyoanzia wilayani Lushoto.

No comments