Stars yaangukia pabaya AFCON 2017.. Makundi ya kufuzu 2017




SAFARI ya Taifa Stars ya Tanzania katika mchakato wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) zitakazofanyika nchini Gabon mwaka 2017, inaonekana kuwa ngumu. Hii ni baada ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kuipanga Kundi G lenye vigogo.
Kwa mujibu wa droo iliyofanyika jana Jumatano jijini Cairo, Misri, Tanzania imepangwa kundi moja na mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, Misri, pia wakipewa mabingwa wa mwaka jana, Nigeria na Chad. Huku Morocco, Tunisia zilizokuwa zimefungiwa na CAF nazo zikijumuishwa katika droo hiyo.
Timu 16 zitakazopenya katika hatua hiyo ya makundi ndizo zitakazokwenda Gabon kusaka ubingwa ambao kwa sasa unashikiliwa na Ivory Coast waliotwaa mapema mwaka huu kwa kuilaza Ghana.
Tanzania kwa mara ya kwanza na mwisho kufuzu fainali hizo ilikuwa mwaka 1980 wakati michuano hiyo ilipofanyika Nigeria na kwa miaka zaidi ya 30 imekuwa ikisota kusaka nafasi ya kushiriki tena bila mafanikio.
Makundi ya michuano hiyo ambayo awali ilikuwa iandaliwe na Libya kabla ya hali ya machafuko ya kisiasa kuifanya ijitoe ni kama yafuatavyo;
Kundi A: Tunisia, Togo, Liberia, Djibouti
Kundi B: Madagascar, DRC, Angola, CAR
Kundi C: Mali, Equatorial Guinea, Benin, South Sudan
Kundi D: Burkina Faso, Uganda, Botswana, Comoros
Kundi E: Zambia, Congo, Kenya, Guinea Bissau
Kundi F: Cape Verde, Morocco, Libya, Sao Tome
Kundi G: Nigeria, Misri, Tanzania, Chad

No comments