Rekodi hizi kali zinasubiriwa kuvunjwa pambano la watani



PAMBANO la watani wa jadi wa soka nchini Simba na Yanga la Machi 8 mwaka huu, lilikuwa ni pambano la 79 kwa wapinzani hao katika Ligi Kuu ya Tanzania katika muda wa miaka 50.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0. Bao lililofungwa na Mganda Emmanuel Okwi na lilikuwa ni bao la 164 baina ya timu hizo tangu zianze kukutana mwaka 1965 katika ligi hiyo maarufu kwa sasa kama Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Siyo kwamba timu hizo hazijawahi kukutana zaidi ya mechi hizo la. Zimeshakutana kwenye mechi za Ligi Kuu ya Muungano iliyoasisiwa mwaka 1982-2014. Pia, zimeshakutana kwenye Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (sasa Kagame) na michuano ya Kombe la Tusker.
Wameshaumana kwenye michuano ya Kombe la AICC, Hedex, Kombe la Mapinduzi, Ngao ya Hisani na hata katika mapambano ya kirafiki kama ile iliyopigwa jijini Mwanza mwaka 2003 na Yanga kuishindilia Simba mabao 3-0.
Kwa kifupi timu hizo zimeshaonyeshana sana kazi katika mechi mbalimbali, lakini katika Ligi Kuu zimeshakutana mara 79 na Yanga kushinda mechi 29 na kupoteza 23 na zilizosalia zilikuwa sare.
Katika mechi hizo 79 Yanga imefanikiwa kufunga jumla ya mabao 87, kumi zaidi ya watani zao Simba ambao wamefunga mabao 77.
Mechi hizo za watani zina vituko vingi vinavyokumbukwa ikiwamo timu kususia mechi, tukio la mchezaji kuanguka uwanjani na kuzimia, beki wa Yanga Rajab Rashid ‘Double R’ kuushika mpira akidhani refa amepuliza kipyenga na kusababisha penati. Unajua ilikuwa lini? Oktoba 20, 1990 na Hamis Gaga ‘Gagarino’ alipiga penalti na kukosa na mwishowe Simba ikalala mabao 3-1.
Hata hivyo, kuna rekodi tatu zinasubiriwa kwa hamu na mashabiki kuona vikivunjwa. Mfungaji Bora wa Muda wote, kipigo kikubwa zaidi cha 6-0 na ‘hat trick’ ya mechi hizo za watani hasa katika Ligi Kuu.
KINARA WA MABAO
Kati ya wachezaji wote waliowahi kufunga mabao katika mechi za watani hao wa jadi, hakuna anayemfikia rekodi ya Omar Hussein ‘Keegan’.
Mshambuliaji huyo nyota aliowahi kuzichyezea timu zote mbili kwa nyakati tofauti, ndiye kinara wa kufunga mabao mengi katika mechi hizo za watani.
Keegan kwa sasa ni kocha alifunga jumla ya mabao sita ambayo hayajaweza kufikiwa na yeyote mpaka sasa licha ya kustaafu soka kitambo kirefu. Keegan aliyafunga mabao hayo akiwa na Yanga aliyoichezea kwa karibu miaka 10 kabla ya kuhamia Simba.
Next

No comments