MANCHESTER UNITED ILIVYOPELEKA KILIO KWA MANCHESTER CITY.. Haikamatiki kwa sasa


Wachezaji wa Manchester United wakishangilia baada ya ushindi wao wa 4-2 dhidi ya Manchester City.
Ashley Young akifunga bao la kwanza kwa Man United dakika ya 14.
Marouane Fellaini akiifungia Manchester United bao la pili dakika ya 28.
Juan Mata akishangilia baada ya kufunga bao la tatu.
Sergio kun Aguero akifunga mojawapo ya mabao yake dhidi ya Man United.
Chris Smalling akifunga bao la nne kwa Man United.
Beki wa City, Kompany akikwaana na Blind wa United.

KIKOSI cha Manchester United kimeiangushia kichapo cha mabao 4-2 Manchester City katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyopigwa leo katika Uwanja wa Old Trafford jijini Manchester.
Mabao ya United yaliwekwa kimiani na Ashley Young dk 14, Marouane Fellaini dk 28, Juan Mata dk 67 na Chris Smalling dk 73 huku mabao ya City yote yakifungwa na Sergio kun Aguero dk ya 8 na 89.
Vikosi:
MANCHESTER UNITED (4-1-4-1): De Gea, Valencia, Smalling, Jones (Rojo 75), Blind, Carrick, Mata (Di Maria 81), Ander Herrera, Fellaini (Falcao 83), Young, Rooney .
Waliokuwa benchi: Da Silva, Januzaj, Valdes, McNair.
MANCHESTER CITY (4-4-1-1): Hart, Zabaleta, Kompany (Mangala 46), Demichelis, Clichy, Jesus Navas (Lampard 73), Toure, Fernandinho, Milner (Nasri 63), Silva, Aguero.
Waliokuwa benchi: Fernando, Dzeko, Kolarov, Caballero.

No comments