Haruna Niyonzima amwagiwa sifa
Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima
KOCHA wa Yanga, Hans Van Pluijm, amesema kiungo wake Haruna Niyonzima ameonyesha mabadiliko makubwa msimu huu tofauti na msimu uliopita ambapo alikuwa akipoozesha mchezo mara nyingi.
Niyonzima alikosekana katika kikosi cha Pluijm kwa
karibu mechi zote za mzunguko wa pili wa msimu uliopita baada ya kocha
huyo kudai kuwa amekuwa akipoozesha mchezo hivyo kupendelea kumtumia
Mrisho Ngassa katika nafasi yake, lakini msimu huu amekuwa hakosekani
katika kikosi cha Mholanzi huyo.
Kocha huyo wa zamani wa Hearts of Ouk ya Ghana
alisema Niyonzima amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi chake kwa sasa
kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufuata mipira nyuma na kupandisha
timu.
“Ni mchezaji wa kiwango cha juu, anajua kucheza na
mpira na kutembea uwanja mzima, amekuwa na mchango mkubwa sana kwetu
kwa sasa,” alisema Pluijm
“Ukiwa kocha unahitaji aina ya wachezaji kama
yeye, ni mchezaji anayeweza kukupa kitu unachokihitaji kwa wakati
wowote, anatengeneza nafasi nyingi kwa wenzake,” alisema Pluijm.
Post a Comment